Makonda Kuzungumza na Wadada Walioumizwa Kimapenzi – Video

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  amesema kuna mpango wa kuanzisha kanzidata (database)  ya ndoa zote zilizopo kwenye mkoa wake ili kupunguza utapeli wanaofanyiwa wanawake kwa kudanganywa kuolewa.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Makonda amesema kanzidata hiyo itahusisha usajili wa ndoa zote ili wanaume waliooa waweze kubainika na kuwanusuru wanawake wasitapeliwe na kuumizwa mioyo kwa kutegemea ndoa.

 

Makonda amesema pamoja na kanzidata hiyo atatumia mkutano wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyiuka nchini ii  kupata uzoefu kutoka kwa nchi nyingine kufahamu namna gani wanakabiliana na utapeli wa aina hiyo.

 

Amesisitiza kwamba kumekuwepo na malalamiko mengi ya wanawake kuumizwa, hivyo wakati umefika wa kuanza kushughulikia tatizo hilo.

 

“Tutaanza kuangalia na kupata uzoefu kwa wenzetu wa SADC ambao mambo kama haya wanashughulikiaje na mkutano ukiisha tutajadiliana kama mkoa tunawezeshaje usajili huo,” amesema.

 

“Kanzidata hii itawasaidia wanawake wasitapeliwe, mtu akitaka kukuoa utaenda mtandaoni na kuangalia taarifa zake, utabaini kama ameoa au la na vilevile itawasaidia hata wanawake ambao wameolewa ili kuzuia waume zao wasioe kwa siri,” ameongeza.

 

Toa comment