Makonda Kusaidia Matibabu ya Moyo kwa Watoto 60 – Video

TAASISI ya moyo ya Jakaya Kikwete, imemmwagia pongezi za kutosha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkonda kwa mchango wake mkubwa wa kujitolea kuwalipia matibabu ya moyo watoto wapatao 60 waliokuwa wakisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu.

Tangu mwezi wa saba mwaka huu, Makonda amekuwa akiwawezesha watoto zaidi 10 kupatiwa matibabu ambapo kati yao tayari walishapatiwa matibabu huku wengine 30 wakiendelea kutibiwa katika taasisi hiyo, ambapo mmoja wa madaktari wa kitengo hicho amesema ndani ya mwezi huu wote watakuwa tayari wamepata matibabu.

Toa comment