The House of Favourite Newspapers

Tazama Live: Walichokisema RC Makonda na Kamishna Awamu ya Tatu ya Oparesheni ya Kupambana na Madawa

Baadh ya wageni waalikwa wakiwa wamekaa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Viongozi wa Majeshi ya Usalama hapa nchini wakiwa kwenye ukumbi huo kusubiri kuanza kwa mkutano.

Viongozi wakibadilishana mawazo

Viongozi wa dini wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.

Moja kwa moja kutoka Ukumbia wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye muda si punde ataanza kuzungumza na wageni aliyowaalika pamoja na wanahabari kuhusu awamu ya tatu ya sakata la madawa ya kulevya.

Miongoni mwa waliofika kwenye mkutano huo, ni msanii TID.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar akitambulisha viongozi mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Dar , Paul Makonda akiwa kwenye Meza Kuu pamoja na Bw.Rogers William Sianga ambaye ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya aliyeapishwa jana na rais Magufuli  Kushoto ni Kamanada wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Soimon Sirro.

Alhadi: Ukiwa kiongzi muadilifu, ukipendwa na mwenyezi Mungu na malaika wake inatosha, ukitaka kupendwa na watu wewe utakuwa zaidi ya Yesu.

Sheikh Alhadi: Mapambano ya dawa za kulevya yanahitaji kumtanguliza Mungu

Sheikh A. Mussa: Tunataka viongozi walio tayari kuchukua maamuzi magumu katika kusimamia haki bila kumwangalia mtu usoni

Makonda akizungumza.

Alhadi: Tunataka viongozi ambao wako tayari kusimamia haki kama alivyosema mheshimiwa Rais na baraka itamiminika katika nchi yetu.

Askofu: Haki kutendeka si jambo jepesi. Haki ni kuleta amani na utulivu. Mungu ndiye msimamizi wa mambo yote ya haki

“Sisi Viongozi wa dini tunaunga mkono jitihada za Serikali dhidi ya dawa ya kulevya”-Mwakilishi madhehebu ya kikristo

Askofu: Tunawakia hekima viongozi wetu katika maamuzi ya haki, Tunaunga juhudi hizo zinazoendelea katika nchi yetu. KKKT tunaye mchungaji ambae ameanzisha juhudi hizi. Naomba mkuu wa mkoa umshirikishe sana mchungaji huyu.

KAMANDA SIRRO: “Nampongeza Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda kwa jitihada juu ya vita hii ya dawa za kulevya…”
Kamanda Sirro: Taarifa ya operesheni tuliyoifanya wiki ya tatu iliyozinduliwa na mkuu wa mkoa Paul Makonda, lengo ni kuwakamata wote wanaojihusisha na biashara hii ya madawa ya kulevya. Mkuu wa mkoa aliunda kamati ya kufanya upelelezi. Watuhumiwa waliokamatwa ni watuhumiwa 311 na vielelezo. Kete 544 za heroin, Mirungi bunda 21.

Kamanda Sirro: Watuhumiwa 117 wamekutwa na vielelezo, 194 hawajakutwa na vielelezo. Watuhumiwa 77 walitakiwa kuja baada ya kutajwa na mkuu wa mkoa. Hadi jana watuhumiwa 32 wameripoti na kuhojiwa, watuhumiwa 45 hawajaripoti na juhudi zinafanyika kuwapata.

Kamanda Sirro: Amabao hawajaripoti watasakwa popote walipo na kupelekwa mahakamani.

Kamanda Sirro: Watuhumiwa wengine upelelezi unaendelea. Pongezi za dhati kwa mkuu wa mkoa kwa ushiriki wake binafsi ya kuongoza mapambano haya. Ukishakuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni vizuri kwenda kwenye ground uone kazi zinazofanyika.

Kamishna Sirro: Wote waliotakiwa kufika kituo cha polisi na hawakufika, watatafutwa na watahojiwa, hilo halikwepeki.

Kamishna Sirro: Kuna wengine wakubwa hawakuamini kama watalala mahabusu, ila walilala, tukikuhoji hatukuachii sababu utaharibu utaratibu.

Kamishna Sirro: Hakuna mtu aliye juu ya sheria hata ukiwa na ukubwa kiasi gani. Nashukuru wengine wameanza kujisalimisha wenyewe.

T.I.D: Niko tayari kujiunga katika vita hii dhidi ya dawa za kulevya, na sitarudi nyuma, namuomba Mwenyenzi Mungu anisaidie.

T.I.D: Ninaamini kuwa muziki bila dawa za kulevya inawezekana.

T.I.D: Ambao mnasema mimi nitakuwa ‘snitch’ kuwa nitawataja, endeleeni kujificha, mimi nimeamua kuingia kwenye vita hii sitarudi nyuma.

Wazazi ambao watoto wao wameadhirika na dawa za kulevya, ndio wanaoelewa vita hii tuliyoianza- RC Makonda.

Makundi ya wanaopiga kelele; 1. Mnufaikaji 2. Walipata kula kupitia wauzaji 3. Watumiaji 4. Wasioelewa kitu- RC Makonda.

Ramadhani Madabida(CCM Dar): Chama hiki ndo kinatawala na kuongoza nchi hii. Tumeomba ridhaa yenu kuwaongoza kupitia ilani.

Madabida(CCM): Ktk Ilani yetu ya Uchaguzi mwaka 2015, ukurasa wa 197 tuliahidi kupambana na matumizi ya Dawa za Kulevya.

Madabida(CCM): Niko hapa kushuhudia kama tuliyoahidi ktk Ilani yanatekelezwa! Tunatakiwa kuiunga mkono Serikali katika mapambano haya.

RC Makonda: Vita hii inakupunguzia idadi ya marafiki, inatia hofu kwako na waliokuzunguka. Si vita ndogo! Rais ana dhamira ya dhati.

RC Makonda: Kuna wanaopiga kelele… Wengine ni wanufaika, kuna waliopata kura na fedha za kampeni kupitia Wauzaji wa Dawa za Kulevya.

RC Makonda: Wapo pia wanaopiga makelele mitandaoni na mitaani kwakuwa hawajui maana ya vita hii au wanafikiria kisiasa.

RC Makonda: Leo ninayo majina mengine 97. Wapo wanaotaka kuhakikisha tunapotea njia; shida yetu ni kuondoa Dawa za Kulevya Dar, basi.

Makonda: Sheria iko wazi. Mtumiaji wa Dawa za Kulevya ni JELA miaka 3. Tatizo watu hawajaisoma sheria hiyo.

RC Makonda: Wengine wanaotumia Dawa za Kulevya wamejikuta wakishiriki mapenzi ya jinsia moja. Kinyume kabisa na misingi ya utu.

RC Makonda: Watanzania takribani 296 wameshakamatea South Africa wakihusishwa na Madawa ya Kulevya.

RC Makonda: Kwa sasa wauzaji wa Dawa za Kulevya wanatumia Mitungi ya Gesi. Hapa Dar zipo takribani bandari bubu 50.

RC Makonda: Leo usiku mtausikia moto utakaowaka ktk viunga vya jiji la Dar. Zipo nyumba takribani 200, nyingine za wanasiasa.

RC Makonda: Kuna Club takribani 20 ambazo zinatumiwa kuuza #MadawayaKulevya jijini Dar. Vipo vijiwe 107 vinavyofanya hivyo.

RC Makonda: Jijini Dar wapo kina mama wanauza vitumbua na ni wauzaji wakubwa wa #MadawayaKulevya.

RC Makonda: Kuna “Bureau de Change” zinazotakatisha fedha za Wauzaji wa Dawa za Kulevya. Wanafanya hivyo kwa kutumia USD.

RC Makonda: Jijini Dar zipo “Bureau de Change” nyingi sana na nyingine zinafanya miamala ya hadi $3,000,000 kwa siku!

RC Makonda: Umri wangu unaniruhusu kujaribu kila kitu! Usilete mbwembwe kwenye utawala huu. Ukiitwa Polisi nenda, acha mbwembwe.

RC Makonda: Kuna wanaofanya biashara hizi si rahisi kuwakamata! Wanaficha sana njia wanazotumia ila wote tumeshawabaini.

RC Makonda: Mtikisiko utakaotokana na Daraja la 3 litapandisha joto. Linahusisha uongozi wa Awamu ya Tatu! Linahusisha makundi mengi.

RC Makonda: Tunapomwita mtu ktk kadhia hii ya #DawaZaKulevya basi ujue tunakufahamu kwa takribani miaka 10 iliyopita! Ujumbe umefika.

PICHA NA DENIS MTIMA: GLOBAL PUBLISHERS

Save

Comments are closed.