The House of Favourite Newspapers

Makonda: Mchungaji Aliyemzalisha Mwanafunzi na Kumtelekeza Akamatwe

RC Makonda akiwa na maofisa wa jeshi la polisi.

 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuagiza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa kumtia mbaroni kiongozi wa dini (mchungaji) anayedaiwa kuzaa watoto wawili na mwanafunzi aitwaye Selina, kisha kumtelekeza.

 

Makonda ameyasema hayo leo wakati Feb. 10, 2018 wakati akitatua kero za wananchi wa Dar es Salaam alipokuwa akifanya mkutano nao katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar na alipoagiza mchungaji huyo akamatwe kabla ya kesho Jumapili.

“Jambo moja limenifedhehesha, naomba RPC Salum Hamdani umjulishe Lazaro Mambosasa, namhitaji huyu mchungaji aliyekatisha ndoto za huyu mwanafunzi na kumpa ujauzito mara mbili. Amefika akaomba msaada akamrubuni akampa mimba, amerudi tena amempa mimba ya pili. Mtu tunayemtegemea atupeleke mbinguni anatupeleka motoni, hawa ni mawakala wa shetani.

 

“Tumeona yaliyotokea kwa ‘Nabii Tito’ anapiga pombe huku anatembea na Mke na mfanyakazi, hana hata aibu, kuna watu wanalitukanisha jina la Kristo, wanajitangaza kuwa Watumishi wa MUNGU kumbe ni Washetani, watu wa namna hii tusiwavumilie turipoti kwenye mamlaka mapema.

 

“Ameshampa mimba mwanafunzi halafu anapata wapi ujasili wa kusema BWANA YESU ASIFIWE? Nataka akamatwe kabla ya Jumapili kufika, ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Makonda.

VIDEO: MSIKIE MAKONDA AKIFUNGUKA

Comments are closed.