Makonda: Mtoto wa Mbowe ana Corona – Video

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema Mwenyekiti Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesitisha mpango wake wa kuitisha mikutano ya hadhara nchi nzima iliyokuwa imepangwa kuanza Aprili 04, 2020 baada ya mwanae kuugua Corona.

 

Amezungumza hayo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika ziara yake ya kukagua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuangalia utendaji wa kazi na ukaguzi wa abiria wanaoingia nchini.

 

Makonda pia amefanya ziara katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo na bandari ya Dar es Salaam ambapo abiria wanasafiri kwenda Zanzibar – Dar.

 

“Kama Mbowe asingepata mgonjwa wa Corona angeingiza Taifa hili katika mgogoro mkubwa, Serikali inasema hakuna mikusanyiko yeye anasema tunakusanyika, Mungu katusaidia kutufikishia taarifa ya umuhimu wa ugonjwa huu nyumbani kwake,”

 

Tusicheze na uhai wa binadamu tuwe sehemu ya serikali katika kuokoa maisha ya Watanzania katika kupambana na janga hili la virusi vya corona.

 

“Ndege kabla haijawasili uwanjani inakuwa na mawasiliano na uwanja husika kama kuna abiria anachangamoto waweze kumpatia msaada mapema afikapo uwanja wa ndege,” amesema Makonda.

 

Pia Makonda amesema kunawatu hawapendi kunawa mkono mara kwa mara kwaajili ya kujikinga na virusi vya corona ili visisambae kwa haraka endapo watanawa mikono kwa sabuni na maji yanayo tiririka.

 

“Tunamshukuru Mungu mpaka sasa hakuna sababu ya kuogopa kinachotakiwa kujikinga ili usipate maambukizi ya virusi vya corona lakini tuendelee kufanya kazi kama kawaida huku tukichukua taadhali” amesema Makonda.

 

Hatahivyo amesema lleo asubuhi Kuna zaidi ya abiria mia mbili walitakiwa waende Comoro lakini wameshindwa kwenda kwa sababu nchi hiyo imesitisha kuingia wageni kutoka nje ni kwaajili ya kujikinga na virusi hivyo.

 

Sanjari na hayo Makonda amesema idadi ya wageni wanaotoka nje ya Tanzania imepungua kwa sababu ndege iliyokuwa inabeba abiria 250 kwasasa inabeba abiria 20 ambayo ni zaidi ya asilimia themanini. Amesema waandishi wa habari ni muhimu sana katika kupambana na virusi vya corona kwani wao ni daraja kati ya wananchi na serikali kwa kupitia wao wananchi wanapata elimu.

 

“Bandarini kama hapa ni muhimu sana maana mnapokea wageni wa kutoka nje ya Nchi au Zanzibar, tujikinge, na wale wanaovaa vitambaa mdomoni havizuii corona ni urembo tu, corona ipo na inaua siwatishi, ukikubali waganga wa kienyeji kazi kwako,” 


Toa comment