The House of Favourite Newspapers

 MAKONDA: Picha za AMBER RUTTY Zinaongeza Joto DSM – Video

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wasanii wote wenye mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamii pamoja na Watanzania ambao wanatumia smartphones, kutumia mitandao ya kijamii kusambaza picha za uzinduzi wa chaneli mpya ya utalii nchini badala ya picha za picha za utupu za msanii Nascat Abubakar ‘Amber Rutty‘ ambazo amedai zinaongeza joto jijini Dar es Salaam.

 

Makonda amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa chaneli ya Utalii ‘Tanzania Safari Channel’ katika Makao Makuu ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mikocheni jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi, Desemba 15, 2018 ambapo mgeni Rasmi alikuwa Majaliwa.

 

Aidha, Makonda amemuomba Waziri Mkuu Kassim, Majaliwa kuruhusu waananchi na watalii kupiga picha kwenye maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam isipokuwa eneo la Ikulu.

 

Makonda amesema kuwa amekuwa hafurahishwi na namna watanzania na wageni wanavyokamatwa pindi wanapopiga picha kwenye maeneo mbalimbali hasa jijini Dar es Salaama jambo ambalo amesema kuwa halina afya katika kukuza utalii na fahari ya nchi.

 

Akitolea mfano katika mataifa yaliyoendelea Makonda amesema kuwa Ikulu kama ya Marekani imejulikana zaidi kutoka na watu kuruhusiwa kupiga picha.

 MAKONDA – Picha za AMBER RUTTY Zinaongeza Joto DSM

LIVE: UZINDUZI WA CHANNEL YA UTALII ‘TANZANIA SAFARI CHANNEL’

Comments are closed.