The House of Favourite Newspapers

RC Makonda Atangaza Neema Ya JPM Kigamboni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia) akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abubakar M. Kunenge (katikati mwenye kofia) pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, Ng’wilabuzi Ludigija wakikagua ujenzi wa jengo jipya la Manispaa ya Kigamboni.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemshukuru Rais Dk John Magufuli ‘JPM’ kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 90 za ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwenye Wilaya ya Kigamboni.

 

Barabara hiyo inaanzia Kibada kuzunguka Mwasonga na Kisarawe Two ikiwa ni sehemu ya kutatua kero za ubovu wa barabara kwa wananchi wa wilaya hiyo.

 

Makonda ameeleza hayo leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Kigamboni na kueleza kuwa Serikali imedhamiria kufanya Mji wa Kigamboni kuwa wa kisasa.

Katika ziara hiyo, Makonda ametembelea ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni lenye thamani ya shilingi bilioni 5.3 ambapo amewataka TBA kuhakikisha wanakamilisha jengo hilo kabla ya Desemba 30 na kubainisha kuwa jengo hilo ndilo jengo kubwa kuliko majengo yote ya halmshauri hapa nchini.

Aidha, Makonda ametembelea ujenzi wa Majengo 7 ya Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni ambayo ujenzi wake umekamilika na kugharimu shilingi bilioni 1.5 hivyo kupongeza manispaa hiyo kwa kukamilisha ujenzi huo mapema.

Stori na Neema Adrian | GPL

“RPC UMLIPE HUYU MAMA MIL 15, HUYO GADDAF YUKO WAPI KWANI? – JPM

Comments are closed.