The House of Favourite Newspapers

Makongoro Oging’ kuagwa leo Dar

0

makongoroMwandishi Makongoro Oging enzi za uhai wake.

ELVAN STAMBULI, Amani

MWILI wa mwandishi mahiri wa habari za uchunguzi, Makongoro Oging unatarajiwa kuagwa leo katika Hospitali ya  Amana  jijini Dar es Salaam kuanzia saa 6 mchana.

Mara baada ya kuagwa na ndugu, jamaa na marafiki, mwili huo utasafirishwa kupelekwa kijijini kwao Marasibora, Tarime mkoani Mara kwa mazishi.

Akizungumza na wafanyakazi wa Global Publishers katika ofisi za gazeti hili juzi Bamaga Mwenge Dar, kaka mkubwa wa marehemu, George Oging’ alisema ndugu yake alizungumza naye siku ya Alhamisi jioni lakini alikuja kupigwa na butwaa baada ya kuambiwa Jumamosi jioni kwamba alizidiwa hivyo alikimbizwa hospitali.

Hata hivyo, baada ya muda mchache aliambiwa na waliomkimbiza Hospitali ya Amana kuwa mdogo wake alifariki dunia.

“Kwa niaba ya familia napenda kuwashukuru viongozi na wafanyakazi wote wa Kampuni ya Global Publishers kwa kutufariji kwa njia mbalimbali tangu msiba huu utokee, hakika tupo pamoja na Mungu awabariki sana,” alisema kaka huyo wa marehemu.

Siku ya Ijumaa, Makongoro alizungumza na wafanyakazi wengi wa Global akiwemo Mkurugenzi Mtendaji, Eric Shigongo aliyemwambia kama hakuridhishwa na matibabu abadilishe hospitali lakini alisema aliendelea vizuri na kwamba alikuwa na uhakika  wa afya yake kuwa nzuri.

Makongoro alikuwa akisumbuliwa na malaria, U.T.I lakini kifua chake kilionekana kina matatizo baada ya kufanyiwa vipimo Ijumaa iliyopita na akapewa dawa za kutumia.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, amina.

RATIBA YA MAZISHI

Saa  2-5              Huduma ya chai na chakula nyumbani kwake  Tabata – Magengeni.

Saa  5-6               Wafiwa kutoka Tabata kwenda Amana Hospitali.

Saa  6-7.30        Ibada fupi na kuaga mwili Amana  Hospital.

 Saa  8-00          Wafiwa kuanza safari kuelekea Marasibora -Tarime.

Mei 28, 2016   Mazishi kufanyika kijijini Marasibora-Tarime.

Leave A Reply