Makosa yanayosababisha wanawake wasiolewe!

WAHENGA huwa wana misemo yao ile kwamba sijui kuolewa ni bahati, kuolewa ni tabia na mingine mingi tu. Leo nataka tujadili juu ya makosa ambayo wanawake wengi wanayafanya na kujikuta wakishindwa kuolewa.  Wanawake wengi wamekuwa wakikwama kuolewa bila kujua sababu ni nini. Au hata kama wanajua kuna ile hali fulani ya ubishi, ujeuri ambao unachangia wajikute hawaingii kwenye mikono sahihi ya waoaji. Wanaambulia kutumiwa na kuachika.

UJEURI

Ndugu zangu, kama kweli wewe unahitaji kuolewa basi jitahidi sana kuepuka masuala ya ujeuri. Unatakiwa kusikiliza, kutafakari kwa makini kile unachoelezwa na kujua nini unapaswa kumjibu mtu ambaye ni mwanaume wako.

Wanaume wanapokuwa kwenye hatua za awali, wanapokutathimini na kukuona ni mjeurijeuri huwa mara nyingi hawapendi kupoteza muda. Wanakuacha na ujeuri wako, wanahamia mahali pengine ambako wanaona watakuwa salama zaidi.

Tabia hii ya ujeuri inaonekana zaidi kwa wanawake ambao kwa namna moja au nyingine wanajiona wana kila kitu. Wana kazi, wana maisha mazuri basi mwanaume kwake si lolote si chochote. Awepo sawa, asipokuwepo sawa, hawa ndio wanaokuwa wajeuri na mwisho wa siku hawaolewi.

UJUAJI

Mwanamke unatakiwa kujishusha, acha kujiona unajua kila kitu kwani wanaume wengi hawapendezwi na jambo hili. Unapojifanya unajua sana, wanaume watakuangalia tu na kukudharau. Mwanamke uwe na haiba ya kike, usipende sana mashindano.

HAKI SAWA

Kupenda haki sawa wakati mwingine ni tatizo, usipende sana kuwa juu ya mwanaume kwani haitakusaidia zaidi ya kukuharibia. Wewe kama mke mtarajiwa basi kweli uwe wa kwanza kujishusha kwa mwanaume wako.

Baadhi ya wanawake wamekuwa wazito sana kuwaheshimu wanaume wao. Ndugu zangu, mnaposhindwa kuwaheshimu wanaume zenu mnataka mkawaheshimu kina nani wengine. Mwanamke ukimheshimu mume wako inalipa asikudanganye mtu.

Huwezi kuonekana mjinga kwa mashoga, majirani au watu mtaani eti kwa kuwa unamheshimu mwanaume wako. Sanasana watu wakikuona unamheshimu watakupongeza, watakusifia sababu huyo ni mwanaume wako, mheshimu.

Ninaposema mheshimu, hii ndiyo asili yetu sisi kama Waafrika na siyo utumwa bali ni misingi iliyokuwepo tangu na tangu. Kwa wale ambao wanasoma Kitabu Kitakatifu cha Biblia, naamini wanafahamu juu ya msingi wa neno hili la kuwaheshimu wanaume. Kitabu cha Wakolosai sura ya 3, mstari ule wa 18 hadi 19 kimeandika: Enyi wake watiini waume zenu, kwani ndivyo apendavyo Bwana, nanyi wanaume wapendeni wake zenu, na msiwe wakali kwao.”

Kumbe basi, mwanamke kumtii mwanaume ni jambo linalomfurahisha Bwana. Unamfurahisha Mwenyezi Mungu sasa ni nani hataki kumfurahisha Mwenyezi Mungu? Au ni nani anayetaka tu kuwafurahisha wanadamu halafu akamchukiza Mungu?

Hakika hakuna awaye yeyote anayeweza kufanya hivyo, basi mtii mume au mwanaume wako kwani ni jambo linalokupa baraka pia kwa Mungu. Na kwa upande wa wanaume nao, kwenye mstari huohuo wameelezwa hapo kwamba wasiwe wakali. Kitendo cha kuheshimiwa kisiwe silaha ya kumyanyasa, kumuona ni mtu wa daraja la pili au kumdharau, wanaume msifanye hivyo sababu pia tumeambiwa tuishi nao kwa akili.

HOFU YA MUNGU

Hili ni la msingi sana, unapokosa hofu ya Mungu utakuwa mshirikina, mjuaji, mpenda majungu, muuaji, mchoyo, mchukia watu!

 


Loading...

Toa comment