MALAIKA ATAJA SABABU ZA KUWA KIMYA

Diana Exavery ‘Malaika’

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Diana Exavery ‘Malaika’ ametaja sababu ya kuwa kimya kwenye gemu hilo kuwa anaangalia upepo unavyokwenda kwanza kisha ataibuka upya.  

 

Akibonga na Mikito Nusunusu, Malaika alisema kuwa anajua mashabiki wake wanajiuliza kwa nini hasikiki tena kwenye muziki lakini ukweli ni kwamba yupo anaangalia njia nzuri ya kuwafurahisha mashabiki wake.

“Japokuwa nasafiri huku na kule lakini yote hiyo ni kuangalia upepo wa muziki unavyokwenda na ni kitu gani mashabiki wanakitaka kwa hivi sasa kama ni Singeli, Mduara au miondoko mingine yoyote ili niweze kutoka tofauti,” alisema Malaik

Stori: Imelda Mtema

Loading...

Toa comment