The House of Favourite Newspapers

Malaika Cute Aonyesha Maisha Ya Kifahari Yanayoshangaza Mitandaoni!

Sosholaiti maarufu kutoka Tanzania, Malaika Cute

Sosholaiti maarufu kutoka Tanzania, Malaika Cute ameendelea kuvutia macho ya wafuasi wake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuonyesha mtindo wake wa maisha wa kifahari. Kupitia picha na video anazoweka mara kwa mara, Malaika ameonekana akifurahia safari za angani huku akiwa ndani ya ndege za kifahari na kuonekana akipiga pozi za kuvutia.

Katika moja ya picha alizochapisha hivi karibuni, Malaika aliandika ujumbe wenye nguvu: ‘Don’t just exist, live 💰,’ akisisitiza umuhimu wa kuishi maisha kamili na kufurahia kila fursa inayojitokeza.

Ujumbe huo ulioambatana na picha yake akiwa ndani ya ndege, umewafanya baadhi ya watu kutoa maoni mseto. Wakati wafuasi wake wengi wakimsifia kwa kuishi maisha anayotaka, wengine wamemshutumu kwa kuonekana kujionyesha na kutamba na maisha ya kifahari.

Aidha, baadhi ya wafuasi wake mitandaoni wamebaini kuwa kwa muda sasa, Malaika ameonekana akipakia picha nyingi akiwa safarini na ndege, hali iliyowafanya wengine kuhoji iwapo anamiliki ndege binafsi au ikiwa anadhaminiwa na wafadhili wakubwa.

Hata hivyo, Malaika hajatoa ufafanuzi wowote kuhusiana na maisha yake ya angani na badala yake amekuwa akionekana kufurahia maisha bila kujali maneno ya watu.