Malaika na penzi la Diamond, Chegge, rushwa ya ngono

MALAIKA2Leo kwenye safu hii unakutana na mwanadada anayefanya poa kwenye ulimwengu wa muziki Bongo, Diana Exavery ‘Malaika’. Mdada huyu alibanwa na Mwandishi Wetu Mayasa Mariwata kwa maswali 10 na yeye bila hiyana akayajibu kama ifuatavyo;

Ijumaa: Ukiwa nyumbani na mwandani wako unapendelea kuvaa mavazi ya aina gani?

Malaika: Hahaa! Hayo ni mambo ya siri kidogo ila ni lazima nivae kimitego zaidi japo siwezi kusema navaaje.

Ijumaa: Ukishakuwa staa, ni ngumu sana kudumu kwenye uhusiano wa kimapenzi? Wewe unafanyaje ili kulinda penzi lako?

 Malaika: Kikubwa ni uaminifu na kujiheshimu, siyo wote tuna tabia chafu. Mimi nampenda mpenzi wangu na siwezi kumpa nafasi kidudu mtu mwingine.

 Ijumaa: Umefanya kazi na Chegge na ikadaiwa kuwa unatembea naye, ya kweli hayo?

Malaika: (Kicheko) sijawahi kuwa na hisia naye za mapenzi sababu Chegge namheshimu kama kaka yangu, ni maneno tu ya watu.

Ijumaa: Mastaa wengi wanapenda kuolewa kwa dau kubwa, wewe unapenda mahari yako iwe kiasi gani?

Malaika: Mimi nimesha-chumbiwa ila hakutoa pesa bali kwa mila za kwetu za Kihaya kuna vitu alitakiwa kuwapa wazazi na sikupiga hesabu kujua ni kiasi gani japo ni vitu vingi vya thamani.

Ijumaa: Hivi leo Diamond Platnumz akikutokea na kutaka uzibe nafasi ya Zari utakubali?

Malaika: Hahaa sijajua, kwanza sijui warembo wanampendea nini ila mimi itakuwa ngumu kwani nimeshapendwa.

Ijumaa: Kutokana na mvuto wako naamini wasanii wengi wenye majina wanakutaka kimapenzi, unatumia njia gani kuwatosa ili wasikufitini kwenye muziki?

Malaika: Wanaponitokea huwa nawajibu kistaarabu tu kuwa nina mtu wangu na mara nyingi wananielewa.

Ijumaa: Kwa nini unapenda kuvaa vinguo vya kihasara wakati una mpenzi wako, huoni unawatega wanaume?

Malaika: Unajua mimi ni msanii kwa hiyo wakati mwingine nikiamua kuvaa kisanii watu wasinifikirie tofauti.

Ijumaa: Sehemu gani ya mwili wako unaipenda zaidi?

Malaika: Mwili wangu wote naupenda ila zaidi napenda miguu yangu.

Ijumaa: Kuna madai kuwa uliwahi kunasa mimba ukaichoropoa, unalizungumziaje hilo?

Malaika: Mimi sijawahi kutoa mimba na haitotokea, nikipata nitazaa sababu umri unaruhusu.

Ijumaa: Ulishawahi kuombwa rushwa ya ngono katika shughuli zako za kimuziki?

Malaika: Nashukuru sijawahi kukutwa na hilo janga la rushwa ya ngono na kama sijawahi mpaka leo sidhani kama itatokea.


Loading...

Toa comment