visa

Malawi: Mahakama Yatupilia Mbali Rufaa ya Rais Mutharika

MAHAKAMA ya Katiba nchini Malawi imekataa rufaa iliyokatwa na Rais Peter Mutharika ya kupinga hukumu ya mahakama hiyo kumfutia ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu wa Mei 2019.

 

Februari 3, 2020, mahakama hiyo ilibatilisha ushindi wa Rais Mutharika kwa kura chache dhidi ya mpinzani wake, kwa maelezo kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na ukiukwaji wa taratibu na kuamuru uchaguzi mpya kufanyika ndani ya siku 150.

 

Aidha, mahakama hiyo umetupilia mbali madai ya tume ya taifa ya uchaguzi kuwa kufanyika kwa uchaguzi wa marudio itakuwa ni gharama kubwa sana.

Majaji wa Mahakama ya Katiba Malawi walioamua shauri la kurudia Uchaguzi wa Rais na kufuta matokeo yaliyompa ushindi Rais Peter Mutharika, wakiwa wamevalia vesti za kuzuia risasi wakati wa shauri hilo. Majaji hao pia wamekishtaki chama tawala (DPP), kwa kujaribu kuwapa rushwa.

 

Akitoa uamuzi wa mahakama, Jaji Dingiswayo amesema demokrasia ina gharama zake, na haki za binadamu ni muhimu.

 

Uamuzi wa mahakama kumfutia ushindi Mutharika ulifikiwa baada ya uchunguzi uliofanyika kubaini kuwepo kwa matumizi ya wino wa kufuta maandishi (Correctional Fluid & Tippex) vilivyotumika kubadilisha takwimu pamoja na matumizi ya nakala bandia za matokeo.

 
Toa comment