‘Malejendari’ vs Kizazi kipya ‘KK’… vita tamu Imenoga!

DIAMOND-PLATNUMZHaina shaka kwamba, Bongo Fleva sasa inakua. Inaibua vipaji vipya kila kukicha kiasi cha kusababisha ushindani mkubwa na wakongwe ‘malejendari’.

Hii yote ni kwa sababu Bongo Fleva imekuwa biashara kubwa inayohitaji ushindani wa hali na mali kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana kati ya chama tawala (CCM) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Pata kujua kuwa ushindani uliopo kati ya wakongwe na wasanii wapya Kizazi Kipya ‘KK’ ambao wanatumia muda, akili na ubunifu kuliteka gemu. Lakini wakongwe nao wanafurukuta kuonesha ukongwe na uwezo wao hivyo kuifanya vita hiyo kuwa tamu na iliyonoga;

Ambwene-Yesaya-21
AY FT DIAMOND -ZIGO REMIX

Ambwene Yessayah ni lejendari ambaye ana singo nyingi kali kama vile Yule, Leo, Binadamu na nyinginezo. Jamaa amelikamata gemu kwa zaidi ya miaka 15 sasa anakimbizana na vijana wapya. Hivi karibuni ameachia remix ya ngoma yake ya Zigo akimshirikisha Mwanamuziki wa KK, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Navy Kenzo – Kamatia

Hili ni kundi linalounganishwa na wapenzi ambao ni Aika Marealle na Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ ambaye ni muimbaji na mtayarishaji, kundi hili lipo katika upande wa KK ambapo linazidi kufanya vizuri sana kitaifa na kimataifa katika gemu ambapo baada ya kufanya vizuri na Wimbo wa Game kwa sasa linatesa kitaani na wimbo mwingine wa Kamatia.

Don’t Bother -Joh Makini

John Simon naye ni mmoja wa lejendari anayewakilisha Kundi la Weusi tangu kitambo ile akiwa River Camp Soldiers. Aliwahi kubamba na Wimbo wa Chochote Popote kitambo kile lakini bado anaonekana kuendelea kung’aa zaidi na hivi karibuni aliachia Wimbo wa Don’t Bother akiwa na msanii A.K.A wa Sauz.

Utanipenda – Diamond

Staa wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ anaonekana kulikamia soko zaidi ikiwemo na kupata mialiko na tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.Kwa sasa anatesa na Wimbo wa Utanipenda ambao unazungumzia maisha halisi kama endapo atafilisika.

Never Ever – Vee Money

Vanessa Mdee ni mwanamuziki wa kike anayefanya vizuri kwenye gemu akiwa ni KK na sasa anatamba na Wimbo wa Never Ever.

mo musiccccMo Music- Skendo

KK mwingine ni Moshi Katemi ‘Mo Music’ anayetamba na wimbo wake wa Skendo baada ya kufanya vizuri kwenye nyimbo kama vile Basi Nenda, Mazoea na nyinginezo.

Maua Sama- Mahaba Niue

Msanii Maua Saleh Sama ni KK wa kike anayefanya vizuri baada ya kutamba na Wimbo wa So Crazy na Let Them Know. Kwa sasa anafanya vizuri katika Wimbo wa Mahaba Niue.

Ommy-Dimpoz-2Ommy Dimpoz- Achia Body

Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ naye anasimama katika kundi la KK. Alitambulika kwenye gemu akiwa na Wimbo wa Nai Nai akiwa na Ali Kiba. Mwaka jana aliachia Wimbo wa Wanjera ambao ulifanya vizuri sana. Kwa sasa anabamba na Wimbo wa Achia Body unaosumbua kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga.

Harmonize- Aiyola

Rajabu Abdul msanii kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya Diamond naye anafanya vizuri sana kwa upande wa KK kwani anaonesha wazi anataka kuwaovateki wakongwe. Anabamba kitaani kwa sasa na Wimbo wa Aiyola.

Nako – OG

George Sixtus Mdemu ni mkongwe wa kurap tangu enzi zile za Nako 2 Nako  Soldiers mpaka Weusi ambaye kwa sasa anakimbiza kwenye Top 10 za Kibongo na Wimbo wa Orginal ‘OG’.

MwanaFA- Asanteni kwa Kuja

Hamis Mwinjuma ni lejendari asiyechuja tangu enzi za East Cost Team (ECT) mpaka kufanya kazi kama msanii wa kujitegemea ‘solo artist’. Bado anaendelea kufanya vizuri kitaani na Wimbo wa Asanteni kwa Kuja.

Jux- One More Night

Mwana KK, Juma Mussa Mpolopoto ‘Jux’ mmoja wa wakali wa RnB nchini, amewahi kutamba na nyimbo kama Nitasubiri, Sisikii na sasa na Wimbo wa One More Night.

Jay Moe- Hili Game

Lejendari, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’ alifanya vizuri na Wimbo wa Mvua na Jua, Kama Unataka Demu, Stori Tatu na sasa amerejea tena na singo mpya ya Hili Gemu na imo kwenye Top 10 nchini.

Barakah Da Prince -Siwezi

Baraka Andrew ‘Barakah Da Prince’ naye ni mmoja kati ya KK aliyeanzia kusikika kupitia Wimbo wa Siachani Naye kisha akafanikiwa kupata Tuzo ya Kili kama Msanii Chipukizi wa mwaka 2015, kwa sasa anawatikisa malejendari na Wimbo wa Siwezi.

Chegge – Sweety Sweety

Juma Said ‘Chegge’ ni lejendari ambaye hajawahi kuharibu kwenye nyimbo zake tangu enzi hizo akitamba na nyimbo kama vile Lover Boy, Goodbye, Mwanayumba na nyingine nyingi. Kwa sasa karudi na Wimbo wa Sweety Sweety  kudhihirisha ukongwe wake.

Ali Kiba-Lupela

Anafahamika kama Ali Saleh Kiba ni mmoja wa malejendari wa Muziki wa Bongo Fleva tangu enzi za Cinderella, Sikuoni, Usiniseme, Mac Muga,Mwana  na nyingine nyingi.

Kwa sasa anabamba na Wimbo wa Lupela ambao video yake aliizindua hivi karibuni.Kikubwa na ‘malejendari’ na Kizazi Kipya ‘KK’ ni kufanya kazi nzuri kwa lengo la kukuza na kufikisha sanaa yetu kimataifa.

Loading...

Toa comment