The House of Favourite Newspapers

Mali: Rais Keita Aachiliwa na Wanajeshi

0

ALIYEKUWA Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, aliyekamatwa Agosti 18, mwaka huu na kundi la wanajeshi lililofanya mapinduzi, ameachiliwa huru jana Alhamisi, jeshi limetangaza.

 

Duru za kuaminika zinabaini kwamba mwanaye, Karim Keita, alifaulu kuondoka nchini na kwa sasa yuko ukimbizini nje ya nchi.

 

Baraza kuu la kitaifa, lililowekwa na wanajeshi kuiongoza nchi “linawaarifu wananchi wa Mali na jumuiya ya kimataifa kwamba aliyekuwa rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta, ameachiliwa huru na kwa sasa yuko nyumbani kwake,” CNSP imetangaza kwenye mtandao wa Facebook.

 

Mmoja kati ya ndugu zake ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema IBK alirejea nyumbani kwake katika eneo la Sebenikoro wakati wa usiku.

Credit: RFI

Leave A Reply