MAMA AELEZEA MWANAYE ALIYEZAMA CHOONI, MKONO UKIJITOKEZA JUU

Choo kilichosababisha kifo

Marehemu Michael Komape.

 

ROSINA KOMAPE  aliwatia huzuni watu waliokuwa mahakamani alipokuwa akilia kuomboleza kifo cha mwanaye wa kiume, Michael Komape, aliyetumbukia katika choo cha shimo shuleni kwake nchini Afrika Kusini.

Mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miaka mitano, alipotea baada ya kwenda chooni katika shule ya Mahlodumela Primary School, Jimbo la Limpopo.

 

Uchunguzi ulivyofanywa, uligundua kwamba mtoto huyo alikuwa ametumbukia katika choo cha shimo cha shule hiyo.

 

“Niliweza kuuona mkono wake uliokuwa umetokeza juu lakini sikuuona mwili wake mwingine,” alisema kwa majonzi mama yake.

 

Rosina alisema alikuwa amepigiwa simu na mwalimu mkuu kujulishwa kwamba mwanaye alikuwa ametumbukia chooni.

 

Yeye na mumewe waliamua kumshitaki Waziri wa Elimu ya Msingi ambaye alikana kuhusika na kifo hicho.  Wazazi hao walisema vyoo vilikuwa vimeharibika na havikufaa kwa matumizi ya binadamu.

 

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza (BBC) wazazi hao waliishitaki wizara ya elimu ya Limpopo na mwalimu mkuu, wakidai walizembea au kutotia maanani haki ya wanafunzi kupata elimu ya msingi katika mazingira bora.

 

Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai kifo cha mtoto huyo kilikuwa ajali na si uzembe.  Tukio hilo liliibua hasira kubwa nchini Afrika Kusini ambapo serikali ilisakamwa vikali kwa kutolishughulikia tukio hilo kwa umakini unaotakiwa.

 

Toa comment