The House of Favourite Newspapers

MAMA AMKAANGA WEMA KWA MAKONDA

Mama akiwa na Mwanaye Wema

DAR ES SALAAM: Kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutangaza oparesheni maalum ya kudili na wanaume mashoga, msanii wa filamu, Wema Sepetu atakuwa amekaangwa na mama yake mzazi Miriam Sepetu, baada ya hivi karibuni kufunguka kuwa, mwanaye huyo alikuwa akiishi na wanaume hao tata.  

Kukaangwa huko kwa Wema kumekuja kufuatia maelezo aliyoyatoa Makonda kwa waandishi wa habari juzikati kuwa, hafurahishwi na matendo maovu yanayoendelea kwenye jiji lake na akawataka wananchi kutuma majina ya wanaume ambao ni mashoga ili adili nao.

Kufuatia agizo hilo, chanzo chetu cha kuaminika ambacho ni rafiki wa karibu wa Wema kilidai kuwa, kati ya majina yaliyotumwa mezani kwa Makonda ni pamoja na ya wanaume ambao wanatajwa kuwa ni marafiki wakubwa wa staa huyo. “Unajua watu walikuwa wakisikiasikia tu kwamba Wema anaishi na mashoga kule nyumbani kwake lakini hawakuwa wakiamini.

“Sasa kitendo cha mama yake kukiri kuwa mwanaye alikuwa akiishi na wanaume hao, amemkaanga kwa Makonda, si ajabu akaitwa na kutakiwa kuwaanika wanaume hao. Lakini nasikia kuna wawili majina yao yameshakwenda kwa Makonda, ikibainika ni kweli wanaume hao ni mashoga na walikuwa wakiishi na Wema, lazima atachafuka tena,” alidai sosi huyo.Image result for MAMA WEMA

MAMA WEMA ALISEMAJE?

Mama Wema hivi karibuni aliwahi kusema kuwa, hafugi ujinga na ndiyo maana hata ‘wale’ mashoga waliokuwa nyumbani kwa Wema, Ununio jijini Dar aliwatimulia mbali. “Mimi sipendagi ujinga. Wale mashoga nimewafukuza wote pale, hawapo tena…” alisema mama Wema.

ORODHA YA MASHOGA KWA MAKONDA

Katika kuonesha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam una mashoga wengi, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makonda Jumanne iliyopita, majina ya mashoga wapatao 100 yalikuwa yameshatua mezani kwake tayari kwa kufanyiwa kazi.

“Mpaka sasa nimeshapokea meseji zaidi ya 5,760 na majina ya mashoga zaidi ya 100. Hii inadhihirisha kwamba, wananchi wa Dar hawataki mashoga, bado naendelea kupokea majina ya mashoga,” alisema Makonda.

Mkuu huyo wa mkoa aliamua kuja na oparesheni hiyo baada ya hivi karibuni wasanii wawili, Wema Sepetu na Ruth Abubakar ‘Amber Rutty’ kuachia video zao chafu hali iliyoashiria kumomonyoka kwa maadili kwa kiwango kikubwa katika Jiji la Dar.

Video hizo zilimsukuma Makonda kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram hivi: “Wananchi na wazazi wengi wamekerwa na tabia ya watu kusambaza picha chafu ikiwa ni pamoja na kujiuza kupitia mitandao ya kijamii. “Jambo hili linaendelea kupoteza utu na staha na kwa kuwa mkoa wetu ni miongoni mwa mikoa iliyoathirika na matumizi mabaya ya mitandao, sasa nimeamua kuendesha zoezi la kuwakamata watu wote wanaofanya vitendo hivi vya aibu.”

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

Comments are closed.