The House of Favourite Newspapers

Mama Auawa, Akatwa Nyeti, Achunwa Ngozi – Video

0

MWANAMKE mmoja mfanyabiashara ya mboga na mkazi wa Mtaa wa Msufini, Chamazi Dar es Salaam, Salima Bakari, ameuawa na kukatwa viungo vyake nyeti, nyama ya paji la uso na ziwa la kushoto.

 

Tukio hilo limetokea kwenye msitu wa Hospitali ya Muhimbili uliopo Chamazi, Jumamosi iliyopita.

 

Kufutia tukio hilo, wanahabari wetu walifika kwenye msiba wa mama huyo na kisha kwenda kwenye msitu huo ambao umekuwa ukilalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kuwa kichaka cha uhalifu na maficho ya majambazi.

 

Majirani walio kando ya msitu huo ambao walielezea hofu yao kwamba majambazi wanajificha kwenye msitu huo ambao mara kadhaa wamekuwa wakiwavamia watu kwenye makazi yao na kuwafanyia uhalifu wa aina mbalimbali ikiwa pamoja na kuwabaka wanawake na kuwapora vitu walivyo navyo.

Leave A Reply