The House of Favourite Newspapers

Mama Aungua Na Maharage Hadi Mfupa Unaonekana, Alia Akiomba Msaada – Video

0

Hujafa hujaumbika! Mwanamke Farida Ramadhan (44), mkazi wa Kibamba CCM jijini Dar es Salaam anaishi kwa mateso makubwa, kufuatia tukio la kuangukia sufuria ya maharage yaliyokuwa yanachemka, na kuungua vibaya mkono wake kiasi cha mfupa wa kiwiko kutokeza nje.

Akizungumza na Global TV, Japo amesema siku ya tukio alijihisi kizunguzungu akiwa jikoni, ndipo alipoyaangukia maharage hayo yaliyokuwa yakichemka, na kusababisha akatwe kidole kimoja cha mkono wa kushoto huku akipata majeraha makubwa kwenye mkono huo.

Maisha anayoishi kwa sasa na mumewe ambaye naye ni mgonjwa, ni magumu, anakosa fedha za kununulia dawa za kuosha kidonda pamoja na fedha za kujikimu na kuwaomba Watanzania wamsaidie kwa hali na mali.

Kama umeguswa, unaweza kutuma mchango wako kwa namba 0677 504 561, jina linatokea ARON MPFIZI (Mumewe).

Kutoa ni Moyo!!

Habari @imeldamtema

Leave A Reply