Mama D Hataki Kufia Leba!

UMEINYAKA hii? Kama bado basi taarifa ikufikie kuwa, mama mzaa chema wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ au ‘Mama D’ anasema kuwa, wanaosema ana mimba, basi wasipate taabu kwani ukweli ni kwamba hana na wala hataki kufia leba.

 

Katika mahojiano maalum, Mama D ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, ajibebeshe mimba ili iweje au apendwe na mumewe, Maisara Shamte kwani hata asipozaa ataendelea kumpenda kama kawaida.

 

“Hivi watu wana wazimu? Nitaanzaje kubeba mimba? Kwani sijipendi? Nani anataka kufia leba na umri huu? Kama kupendwa, napendwa sana,” alisema Mama D au Mama Dangote mwenye umri wa miaka 50 ambaye hivi karibuni alidaiwa kuwa ni mjamzito.

Stori: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment