Mama Dangote Amuwakia Shilole “Usirudie Tena”
IKIWA ni siku moja baada ya msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kumchukua dada aliyedai kuwa ni shabiki wa Msanii Diamond Platnumz kutoka Paris nchini Ufaransa na kumpeleka wakapige naye picha, Mama mzazi wa Damond, Bi Sandrah Sanurah maarufu kama Mama Dangote ameonesha kukasirishwa na kitendo hicho.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Mama Dangote ameonyesha kuchukizwa huku akidai kuwa anachokifanya Shilole ni kumpelekea mwanaye wanawake jambo ambalo yeye kama mzazi hajapendezwa nalo, hivyo akome tabia hizo.
“Kama mzazi hakuna anayefurahia kuona mwanae analetewa mwanamke ovyo ovyo bila kuzingatia staha ya mtu kama mtu, au imani zetu. Ukizingatia huyo mtu kashatangaza hadi pesa ili apige picha na mwanangu ila kwa kuwa tunajua nia yake ni ovu hatukumpa nafasi hiyo.
“Mwanangu ni tafsiri halisi ya jamii (kioo cha jamii) yenye nidhamu tofauti na alivyo au ulivyomchukulia, Shilole usirudie tena na siyo maisha kuchukuliana poa watu wakiwa kazini.
“Hakuna msanii anayekubali kila mtu anayesema ni shabiki yake kirahisi… Sisi ni wazoefu wa kushuhudia mashabiki ila siyo huyo au aina hiyo ya shabiki sijapenda Shilole ulichokifanya,” amesema Mama Dangote.