Mama Dangote: Nafurahi Kuona Diamond na Watoto Wake
MAMA mzazi wa staa mkubwa wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz, Sanura Kassim anasema kuwa, anafurahi mno na kuona kama pambe la kufungia mwaka anapomuona mwanawe huyo akiwa na watoto wake, Tiffah Dangote na Prince Nillan pamoja na mama yao, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Mwishoni mwa wiki iliyopita na mwanzoni mwa wiki hii, Diamond au Mondi alikwenda kuitembelea familia yake hiyo iliyopo nchini Afrika ya Kusini na kujiachia nayo ile mbaya.
Katika mazungumzo yake na Gazeti la IJUMAA, Mama Dangote anasema hakuna kitu kinamfurahisha kama anapomuona mtoto wake huyo akiwa na wanawe hao wakienda huku na kule na akiwa na maelewano ya juu kabisa na mama wa watoto hao maana ndicho kitu cha muhimu kwao kama familia.
“Nafurahi sana kuona wajukuu wangu wakiinjoi na baba yao. Kwangu ni faraja na napata usingizi vizuri sana. Naomba iwe hivyo muda wote kwani mimi nafurahi maana wanapata mapenzi kotekote kwa mama na baba na watoto wanapata kitu kizuri, mimi naona pambe tu,” anasema Mama Dangote.
Mbali na watoto hao, pia Diamond amezaa na watoto wawili na wanawake wengine, Hamisa Mobeto na Tanasha Donna.
STORI; IMELDA MTEMA, DAR