visa

Mama Godzilla: wasanii wamenitenga

MAMA wa aliyekuwa msanii wa miondoko ya Hip Hop Bongo, marehemu Golden Mbunda ‘Godzilla’, Marry Challe amefunguka kuwa, wasanii wengi wamemtupa na hawaonyeshi ushirikiano wowote walioahidi katika mazishi ya mwanaye Godzilla.

Mama huyo ambaye hayupo sawa kiafya tangu alipopatwa na msiba huo, amesema kuwa licha ya ahadi nyingi zilizotolewa na wasanii wengi kuwa wataiangalia familia ya Godzilla ikiwa ni pamoja na yeye na mtoto aliyeachwa na rapa huyo, ni Fareed Kubanda ‘Fid Q’ pekee ndiye msanii anayekuwa bega kwa bega katika kipindi chote.

“Ahadi wengi walitoa lakini mpaka sasa anayeonesha ushirikiano ni Fid Q tu wengine sijawaona tangu mazishi, ila ni vyema kama wangejitahidi kutimiza ahadi zao japo siwezi kuwalaumu kwani nao pia ni binadamu inawezekana wamepata dharura au mambo magumu ila ni vyema wakamkumbuka hata mtoto wa marehemu,” alisema mama huyo.

Godzilla alifariki dunia Februari 13, mwaka jana ambapo wasanii wengi waliofika msibani hapo waliahidi kumsaidia mtoto wa marehemu kumsomesha na mahitaji mbalimbali lakini wote wamekuwa kimya

Stori: Qaissy Mohamedy, Amani
Toa comment