The House of Favourite Newspapers

Mama Kanumba Anavyozidi Kuwaliza Bongo Muvi

0

INASIKITISHA! Hakuna neno lingine unaloweza kusemwa mbali na hilo. Wakati muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiendelea kuhudhuria Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo kesi yake anayotuhumiwa kumuua bila kukusudia, Steven Kanumba, baadhi ya wadau wa filamu wamekuwa wakisikitishwa na hali ya maisha ya Mama Kanumba, Flora Mtegoa, ambaye amekuwa akihudhuria kesi hiyo kila siku inapotajwa tangu wiki jana.

Akiwa mahakamani hapo leo Alhamisi, Mama Kanumba alionekana kukosa furaha na kuwa mnyonge kabisa wakati kesi ikiendelea, ambapo huenda anakuwa na mawazo kuhusu alivyokuwa akiishi na mwanaye, na vitu anavyovikosa kwa sasa na pengine angevipata Kanumba angekuwa hai.

Bond.

Muigizaji Bond Bin Sinnan aliyewahi kuwa mpenzi wa muigizaji Wastara Juma, ameandika ujumbe kuonyesha kusikitishwa na jinsi mama huyo anavyoteseka na maisha.

“Siku zote huwa nikikutizama naishiwa nguvu mwilini na amani moyoni mwangu. Huwa najiuliza mengi sana. Nikimtizama Diamond anavyomlea mama yake nakumbuka Steve alivyokuwa anakulea wewe. Nikuombee kwa Mungu azidi kukupa nguvu na ujasiri na uamini binaadamu hajiendeshi bali huendeshwa na Mungu,” aliandika Bond.

Aidha katika kesi hiyo, wazee wa Baraza la mahakama hiyo leo wametoa maoni yao kuwa Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia.

Muigizaji, Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua aliyekuwa muigizaji wa filamu, Steven Kanumba bila kukusudia. Lulu anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7,2012, nyumbani kwa Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Jaji Rumanyika ameiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 13 mwaka huu ambapo Mahakama hiyo itatoa hukumu.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

==

VIDEO: Lulu Alimuua Kanumba Bila Kukusudia – Wazee wa Baraza

Leave A Reply