The House of Favourite Newspapers

MAMA KAWELE ASIMULIA ALIVYOZIMIA LOCATION

Image result for mama kawele
Mama Kawele

GRACE Mapunda siyo jina geni masikioni mwa mashabiki wa filamu za Kibongo. Mama huyu amejizolea umaarufu kutokana na uhalisia anaouonesha kwenye filamu nyingi alizocheza.   

 

Leo Gazeti la Amani limempata na kufanya naye mahojiano ya ana kwa ana ili kujua mambo yake mengi ndani na nje ya filamu na haya ndiyo yalikuwa mazungumzo yetu;

Amani: Grace Mapunda ni jina lako halisi au unalitumia tu kama wanavyofanya wasanii wengine?

Mama Kawele: Grace Mapunda ni jina langu la kuzaliwa ila kuna baadhi ya watu wananifahamu kwa jina la kisanii ambalo ni Mama Kawele.

Amani: Ilikuwaje ukaingia kwenye uigizaji?

 

Mama Kawele: Ni stori ndefu kidogo, mimi kipaji changu ambacho nilikuwa nahisi Mungu amenipa ni uimbaji. Nimeimba sana kanisani na hata familia yangu kwa jumla walikuwa wanajua nitakuja kuwa mwanamuziki wa kudumu milele, lakini hiki kipaji cha pili ambacho kimekuja kuonekana, mtoto wangu wa kwanza ndiye aligundua na hata siku ambayo ananiambia ninafaa kuwa mwigizaji, binafsi sikuwa ninaamini. Lakini kwa kile alichokiona, alijitahidi kusisitiza na kutumia njia tofautitofauti kunishawishi hadi nimekuja kujishtukia nipo ninaigiza kupitia yeye.

 

Amani: Mbali na mwanao kuna msanii yeyote alikuvutia?

Mama Kawele: Yah! Kuna mwigizaji mmoja anaitwa Kemmy wa Kaole. Ni mwigizaji ambaye nilipenda sana alivyokuwa anaigiza.

Amani: Tofauti ya sanaa ya zamani na sasa hivi ni nini?

Image result for mama kawele

Mama Kawele: Tofauti ni kubwa, nimepitia kwenye vikundi na ndani ya vikundi kulikuwa na vitu vingi ambavyo mnakutana navyo kama unavyoona shuleni. Kulikuwa na kujifunza. Kulikuwa na nidhamu, kulikuwa na vitu vingi sana kiasi kwamba msanii ukikaa ndani ya miaka mitatu hadi minne tayari unakuwa kama umetoka darasani na umepata cheti. Lakini sasa hivi wasanii wanaibuka tu ghafla, hawapitii mafunzo ya aina yoyote ndiyo maana kila siku tunasemwa kuwa tunatoa kazi mbaya.

Amani: Sanaa imekunufaisha vipi?

 

Mama Kawele: Kwanza namwambia Mungu asante kwa sababu siyo kila kitu unachokipenda unaweza kukipata. Inawezekana Mungu akakupa kizuri zaidi kuliko kile unachokipenda. Nilikuwa nawaza kuwa mwanamuziki, lakini Mungu akanipa kitu kingine ambacho nasema sasa hivi ni mwigizaji na Watanzania wananifahamu.

Jambo la pili namshukuru Mungu kwa sababu kupitia sanaa imenipa marafiki ndani na nje ya nchi. Mbali na hilo nimeweza kuwa na makazi yangu kupitia sanaa.

Amani: Unadhani ni kwa nini wasanii wengi siku hizi hawachezi sana muvi kama zamani badala yake wamehamia kwenye tamthiliya?

 

Mama Kawele: Tamthiliya zilikuwepo tangu zamani isipokuwa sasa hivi zimeboreshwa. Lakini nchi yetu ilichelewa kufanya tamthiliya kubwakubwa kama sasa ila niseme kuwa tumeanza na tumeona faida ndani ya tamthiliya. Binafsi hata kipato changu kinaongezeka kupitia tamthiliya.

Amani: Filamu gani uliyofanya na ndiyo ilikutambulisha kwa Watanzania?

Mama Kawele: Filamu iliyonitambulisha kwa Watanzania inaitwa Fake Smile ambayo nilifanya na marehemu Steven Kanumba. Nyingine ni Laana, Nasaba, Wrong Richness na nyinginezo.

Amani: Kuna dhana imejengeka kwamba ili utoke kisanaa na ufahamike haraka ni lazima utembee na madairekta, je, kwa upande wako ilikuwaje?

Image result for mama kawele

Mama Kawele: Kwa upande wangu unajua uhusiano sehemu yoyote upo, yaani jinsia mbili zikikutana uhusiano lazima uwepo. Lakini inategemea na wewe mwenyewe unavyojichukulia. Niseme tu ukiwa kama mwanamke, jambo la kwanza thamini mwili wako, jambo la pili, unatakiwa ujitambue, hivyo nilipoingia kwenye sanaa nilijijua mimi ni nani na ninatakiwa kufanya nini mwisho wa siku nikazishinda tamaa na ndiyo maana mpaka leo hii bado nafanya vizuri na sina skendo.

 

Amani: Kitu gani kibaya ambacho kimewahi kukutokea kwenye uigizaji ambacho huwezi kukisahau?

Mama Kawele: Naweza kusema ni kitu cha kawaida ambacho binadamu yeyote humtokea. Nilipata tatizo la kuugua ghafla nikiwa ‘location’. Nilipoteza fahamu wakati naambiwa tu action na dairekta, kichwa kilianza kuniuma sana ila kuna wakati nilikuwa ninajikaza, lakini nilishindwa kwa hiyo mwisho wa siku nilipoteza fahamu kwa saa mbili na baada ya hapo nikaja kuzinduka nikiwa hospitalini.

Amani: Ni changamoto gani huwa unazipitia pindi unapokuwa location?

 

Mama Kawele: Naweza kusema kwamba kwenye nchi yetu tunapigana tafu wenyewe kwa wenyewe bado hatujapata madairekta wenye weledi kwa sababu kuna muda mnakuwa location, dairekta anakwambia ufanye kitu fulani, lakini kwa hali unayoiona, unaona kabisa hapa tunafeli na kikubwa ni madairekta kukosa ushirikiano.

Amani: Ukikutana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harisson Mwakyembe ungependa kumwambia nini?

 

Mama Kawele: Naamini Tanzania kuna vipaji vingi, laiti kama tungekuwa tumebarikiwa kupata madairekta ambao wamesomea kazi ya sanaa, tukapata vifaa kama vile ambavyo wenzetu wa nchi zilizoendelea wanatumia, tukapata location ambazo zinahusiana na stori ambayo tunayo, naamini Tanzania tungekuwa mbali kisanaa.

Amani: Mara nyingi umekuwa ukiigiza muvi za majonzi au ukali, kwa nini sehemu hizo tu?

 

Mama Kawele: Ni scene ambazo nadhani nikipewa nazifanya vizuri, japokuwa watu hawajui tu kuwa mimi ni muoga sana wa kamera na ukweli sijawahi kuzizoea.

Amani: Mama Kawele ni mtu wa aina gani mbali na yule tuliyezoea kumuona runingani?

Mama Kawele: Watu wengi wanamchukulia Mama Kawele ni mama ambaye anapenda kulia au kuna muda mkalimkali hivi, lakini hapana, mimi napenda sana kucheka (anacheka), napenda kupig

Makala: Memorise Richard

Comments are closed.