The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mama Lawamani Skendo ya Sanchi

0

KWA wafuatiliaji wa mitandao ya kijamii, gumzo kubwa lilikuwa ni skendo ya picha za utupu ambazo anadaiwa kupiga au kupigwa, mrembo mwenye shepu ya aina yake Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’.

Lakini pamoja na picha hizo kumhusu Sanchi zaidi, watu mbalimbali walioongea na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, wamemtupia lawama zaidi mama yake mzazi ambaye kitaaluma ni mwalimu.

 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili wakazi wa Jiji la Dar, walisema kitendo cha Sanchi kukwaa skendo hiyo kungeweza kuepukwa kama mama yake angechukua hatua stahiki.

“Mama alipaswa kumuonya mwanaye kwa sababu suala la kupiga picha za nusu utupu hakuanza leo sema hizi mpya amezidisha kwa kupiga utupu zaidi.

 

“Kwa sisi tunaofuatilia Instagram tulikuwa tunapata shida sana kuamini kama huyu dada ana mama yake mzazi kabisa au wazazi wote wawili, sasa kuna wakati akatuchosha zaidi kwa kumposti mama yake,” alisema John Kioo, mkazi wa Sinza, Dar.

Naye Mwanaisha Shaban wa Kimara, Dar, anamhurumia mama Sanchi kwani katika kipindi kama hiki, ataiweka wapi sura yake maana yeye ni mtu ambaye anazungukwa na wanafunzi ambao wanategemea kujifunza kutoka kwake.

 

“Simpatii picha kwa kweli huyo mama maana watoto wenyewe siku hizi haya mambo ya kwenye mitandao wanayaona, wanajua kila kitu sasa hebu angalia wameshaona halafu kesho na keshokutwa watakutana darasani,” alisema.

Mbali na wakazi hao waliozungumza moja kwa moja na IJUMAA WIKIENDA, maoni mengi kwenye Ukurasa wa Instagram wa Global Publishers, nayo yalimtupia lawama bi mkubwa huyo sambamba na familia yake kwa ujumla.

 

“Hivi kweli kama familia hawaoni haya mambo? Sanchi hawezi tu kuwa na mama yake pekee, lazima atakuwa na wajomba, kaka zake, mashangazi na ndugu wengine kweli wote wapo tayari kuibeba aibu hii?” Alihoji jamaa anayejiita Kitaleo huko Instagram.

Maoni hayo mengi yalielekeza lawama hizo kwa mama Sanchi kwa kile walichodai, suala la kupiga na kutupia picha za nusu utupu halikuanza leo katika ukurasa wake wa Instagram.

 

Wengi walisema kama walikuwa wanaona halafu hawamuelezi, basi ni wakati sasa wa kumueleza ukweli kwamba kwa hatua aliyofikia anawadhalilisha hata wao ambao hawafanyi matendo hayo.

Aidha, watu hao walimtaka zaidi mama kusimama imara kama mama na kumuelekeza binti yake misingi mizuri ya maisha na si kumruhusu

 awe anaweka picha za nusu utupu kwenye akaunti hiyohiyo ambayo pia huwa anatupia na picha za mama yake.

 

Watu hao wamesema wanaamini kama mama akisimama imara kama mzazi na kutimiza wajibu wake sawasawa, Sanchi lazima atabadilika maana mbali na kuwa rafiki yake kipenzi, anaonekana ni mtu anayeweza kumsikiliza.

“Wewe unafikiri mama akisema, Sanchi ana uwezo wa kukataa? Kuna mahali tu mama aliteleza ndiyo maana Sanchi akawa anajifanyia mambo ya hovyo tu mitandaoni halafu mama yupo tu,” alichangia mtu aliyejiita Kidani mtandaoni.

 

IJUMAA WIKIENDA lilijaribu kumtafuta mama Sanchi ili kuweza kusikia anazungumziaje skendo hiyo ya mwanaye, lakini jitihada za kupata namba yake ziligonga ukuta baada ya wanahabari wetu kufika katika Shule ya Sekondari ya Zanaki jijini Dar anayofundisha na kushindwa kupata mawasiliano yake kwa kuwa haikuwa siku ya masomo.

Jitihada zaidi za kumpata mama huyo zinaendelea, lakini hata hivyo, kwa upande wa Sanchi kupitia ukurasa wake wa Instagram, amekanusha kuwa picha hizo mpya za utupu zilizosambaa wiki iliyopita si yeye.

 

“Sikutaka hata ku-address hili jambo, lakini nimeona linakua kwa kasi sana. Let me say this clearly, hizo video mnazotumiana huko WhatsApp siyo mimi.

“Jamani msinifananishe na shepu za kawaida mnanikosea. Yaani sijaumbwa hivyo. Take your time kuchunguza utajua tu. Wala hutatumia nguvu nyingi kujua hizo video siyo mimi. Details kidogo tu.

 

“Kuna video nimeona mdada amelala kwenye jakuzi jamani hiyo siyo shape yangu. Hiyo shape ni ndogo mno. Mimi ningelala hivyo ingekuwa hatari ningesambaa sana maana’ke nimejazia zaidi. Jakuzi zenyewe huwa sitoshei nakaa kiupande. Rangi yake pia siyo kama yangu. Na maziwa yangu yamejaa zaidi siyo kama hayo.

 

“Sitetereki wala sitayumbishwa. Kwa wanaojifariji kusema ni mimi darlings am sorry to disappoint you it ain’t me. Nimeposti hili kwa ajili ya watu ninaowapenda wasije kuamini uongo.”

Stori: Mwandishi Wetu, Dar

Leave A Reply