The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mama Mbaroni kwa Kutelekeza Watoto Shambani

0

POLISI mkoani Mwanza imemkamata Happiness Mafuru (23) kwa tuhuma ya kuwatelekeza watoto wake wawili katika majaluba ya mpunga majira ya saa 11 jioni katika Mtaa wa Mtakuja, Nyamhongolo, Wilayani Ilemela.

Watoto hao, Kelvin Mathias (mwaka 1 na miezi 7) na mwingine Anastazia Mathias (miezi 4) waliokotwa saa 9 usiku wakiwa hai na kisha kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando na sasa wanaendelea vizuri.

Aidha, polisi wamebainisha kuwa upelelezi wa kina ili kujua mazingira ya tukio husika yakoje unaendelea pamoja na kuendelea kumsaka mzazi mwenzake na mama huyo ambaye alitoroka.

Leave A Reply