The House of Favourite Newspapers

Mama Mmarekani Atua Nigeria Kufunga Ndoa na Kibenteni, Walikutana Insta

0

MAMA mmoja kutoka California Marekani, Jeanine Delsky (43), amefunga safari mpaka nchini Nigeria nyumbani kwa wazazi wa kijana Sulaiman Babayero (23) kwa ajili ya kufunga naye ndoa.

 

Wawili hao walianza mahusiano yao mwaka jana baada ya kukutana kwenye mtandao wa Instagram na baada ya kutongozana kukubaliana kupitia mtandao huo, mwanamke huyo (pichani) alifunga safari hadi Nigeria kuwaona wazazi wa jamaa huyo na kufanya makubaliano, ambapo Machi mwaka huu (2020) watafunga ndoa kisha kwenda kuishi Marekani.

 

Suleiman ambaye ndo kwanza amemaliza elimu ya Sekondari, ndiye aliyeanza kumtongoza Mwanamke huyo, na mama huyo alipogundua kijana huyo si tapeli, yupo serious ndipo wakaanza kuwasiliana na kuweka mikakati ya uhusiano wao na maisha yao ya baadaye.

 

Pia, wazazi wa kijana huyo, baba yake amesema atamsapoti mtoto wake kwa lolote ili ndoa yao ifanikiwe huku mama yake aitwaye Fatima Suleiman mama akisema hana tatizo mwanaye kuoa mwanamke mwenye umri mkubwa, zaidi anawatakia ndoa njema na maisha mema.

Leave A Reply