MAMA MOBETO MAMA D, NGOMA DROO

DAR ES SALAAM: Ni mwendo wa kujiachia na wanaume waliowazidi umri (vibenten) au kwa msemo wa watoto wa mjini ni mwendo wa vipara!  Unaambiwa aliyeanza ligi ya kujidai kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ni mama wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitamba kimahaba na mista wake, Maisara Shamte ‘Anko’.

Lakini wikiendi iliyopita ilikuwa ni zamu ya mama wa mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto ‘Misa’, Shufaa Rutiginga ‘Mama Mobeto’ ambaye alifumwa laivu na kamera zetu akiwa na jamaa aliyeonekana kumzidi umri.

NI KWENYE MISS KINONDONI

Tukio hilo lililoshuhudiwa na Risasi Mchanganyiko lilijiri kwenye Shindano la Miss Kinondoni 2019 lililofanyika usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita katika Ukumbi Life Park uliopo Mwenge jijini Dar.

Kufuatia tukio hilo, mama Mobeto ambaye binti yake, Hamisa amezaa na Diamond, alizua gumzo kama lote huku wapenda ubuyu wakidai kuwa alikuwa anajibu mapigo kwa Sandra au Mama Mondi ambaye amekuwa akitrendi ile mbaya na Anko Shamte.

“Jamani huyu si ni mama  Misa (Mobeto)? Naona ameamua kumlipa Mama Dangote (Mama D), naona yupo na kibenten chake anajilia bata zake mdogomdogo. Maisha yanataka nini tena? Kula raha mama kufa kwaja,” alisikika mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

MAMA MOBETO MASHAUZI KAMA YOTE

Hata hivyo, wakati watu wakiwapiga chabo na minong’ono kutawala kila kona ukumbini humo, mama Mobeto alikuwa ni kama ametiwa ndimu maana alikuwa akionesha mashauzi kama yote akiwa na kibenten wake huyo.

RISASI LAMVAA

Katika hali hiyo, Risasi Mchanganyiko lilimvaa mazima mama Mobeto na kumuuliza juu ya kile kilichokuwa kinaendelea huku akijibebisha kwa jamaa huyo ambapo alifunguka.

NI MTU WAKE

Mama huyo alisema kuwa jamaa huyo ni mtu wake wa karibu na pia anamchukulia kama kaka yake.

MSIKIE MAMA MOBETO;

“Mbona limekuwa gumzo jamani? Yaani watu wakikuona umeongozana na mwanaume tu, wanaanza kusema yao! “Ni hivi; huyu ni mtu wangu wa karibu. Pia ni kaka yangu ambaye tunashirikiana kwenye vitu mbalimbali vya kwenye familia na anaitwa Pizzo,” alisema mama Mobeto akiomba aachwe, apewe nafasi aendelee kujiachia na mtu wake kwani alikuwa akipata maji ya kunywa kidogo ili kukata kiu.

NGOMA DROO

Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii, kwa sasa mama Mobeto na mama D ngoma ni droo kwani kila mmoja anakula maisha na mtu wake bila kificho.

Kwa upande wake mama D amekuwa akiachia picha kali za kimahaba akiwa na Shamte huku akisindikizia na maneno ya vijembe. Katika mahojiano yake na gazeti hili hivi karibuni, mama D alitamba kuwa kwa sasa mahaba yake na Anko Shamte ni kama yote.

Risasi Mchanganyiko: Mama D tunaona mahaba yako na Anko Shamte ni motomoto!

Mama D: Kama yote.

Risasi Mchanganyiko: Safi sana safi sana…Mama D…

Mama D: Ndiyo mimi mke halali wa ndoa akitokea mwingine feki.

Risasi Mchanganyiko: Kumbe mlishafunga ndoa?

Mama D: Kama unapajua kwangu uje nikuoneshe cheti cha ndoa.

ANAUA SOO?

Hata hivyo, kuna madai kuwa Mama D amekuwa akijiachia kimahaba na Anko Shamte ili kuua soo la mwanaume wake huyo kudaiwa kuchepuka na kuzaa na mwanamke mwingine anayetajwa kwa jina moja la Sharifa.

 

Toa comment