The House of Favourite Newspapers

Mama Mzazi wa Mbunge wa viti Maalum Halima Mdee Bi.Theresia, Afariki

Mama Mzazi wa Mbunge wa viti Maalum Halima Mdee Bi.Theresia Mdee, amefariki leo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.

Kwa mujibu wa Mbunge Ester Bulaya ambaye ni rafiki wa Halima, amesema Mama huyo ambaye ameugua kwa muda mrefu akipata matibabu katika Hospitali mbali mbali ikiwemo hiyo ya Benjamin Mkapa, amefariki dunia na taratibu zingine za maziko yake yatakuwa wapi zitatolewa hapo baadaye.