Mama Samia Aalivyotua Kwenye Banda la NBC Nanenane – Simiyu

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akimkaribisha Makamu wa Rais, Samia Suluhu (kulia) kwenye banda la benki hiyo lililopo kwenye Maonesho ya 28 ya kilimo na mifugo – Nane Nane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu yakiwa na Kauli mbiu “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020”. Benki hiyo ni moja wa wadhamini wa Maonesho hayo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan ametembelea Banda la Benki ya NBC kwenye ufunguzi wa maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu leo Jumamosi, Agosti 1, 2020.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu (Kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alipokuwa akielezea kuhusu huduma za benki hiyo kwa wadau wa kilimo wakiwemo wakulima wakati Makamu wa Rais alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye Maonesho ya 28 ya kilimo na mifugo – Nane Nane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu yakiwa na Kauli mbiu “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020”. Benki hiyo ni moja wa wadhamini wa Maonesho hayo.

Benki ya NBC imekuwa ni mdhamini wa maonesho haya ya Nanenane kwa mwaka wa tatu mfululizo.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (katikati) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa pili kulia) kwenye banda la benki hiyo lililopo kwenye Maonesho ya 28 ya kilimo na mifugo – Nane Nane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi Mkoani Simiyu yakiwa na Kauli mbiu “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020”. Wengine ni viongozi wa waandamizi wa benki hiyo.

 

 

Toa comment