The House of Favourite Newspapers

Mama Samia Suluhu amuokoa Wastara

0

12039568_1034578279906706_5541940585429705686_nMakamu wa Rais, Mama Samia Suluhu

Hamida Hassan
Msanii wa Filamu, Wastara Juma amemshukuru Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu kwa msaada wake katika matibabu ya awali ya mguu wake licha ya kwamba bado zinahitajika zaidi ya shilingi milioni 10 ili aweze kutembea vizuri.

Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu kutokea Nairobi-Kenya, Wastara alisema katika hatua ya awali ya kutibu mguu wake Mama Samia alimsaidia kiasi fulani cha fedha hivyo anamshukuru sana.

WASTARA1Msanii wa Filamu, Wastara Juma.

“Nimefanyiwa matibabu ya awali ambayo zimetumika fedha nyingi sana, kati ya hizo Mama Samia kanisaidia, hata hivyo ripoti ya daktari inaonesha natakiwa kufanyiwa upasuaji zaidi na kubadilishiwa mguu, natakiwa kuwa na milioni 10 mkononi.

“Najipanga kurudi Bongo kuzitafuta kabla ya kurudi tena hospitalini baada ya miezi mitatu, naamini kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu nitazipata, naomba tu dua zenu ili niweze kuwa sawa,” alisema Wastara.

Leave A Reply