The House of Favourite Newspapers

MAMA WA AMBER RUTTY AVAMIWA AUAWA !

DAR ES SALAAM: Majanga juu ya majanga! Ndivyo unavyoweza kusema, wakati msanii wa Bongo Fleva, Nascat Abubakary ‘Amber Rutty’ akiwa kwenye msala wa kujirekodi na kusambaza video chafu, imebainika kuwa, mama yake mlezi, Halima Ibrahim alivamiwa na kuuawa na watu wasiojulikana, Risasi Jumamosi linakupa habari kamili.

 

BABA AFUNGUKA

Akizungumza na Risasi Jumamosi, baba mzazi wa Amber Rutty, Abubakary Abdul alisema kuwa, mkewe huyo aliuawa kikatili Oktoba 28, mwaka huu, wakati akiwa anajiandaa kuswali swala ya alfajiri eneo la Marekebo, Bomba-Mbili, mkoani Ruvuma.

Alisema watu wasiojulikana walimvamia wakati akiwa ametoka kupata udhu nje ya nyumba aliyokuwa amehamia kwa dharura.“Yaani kama vile walikuwa wanamvizia tu atoke, alipotoka tu kwenda kuweka udhu nje ya nyumba hiyo, wakati anarudi, walijitokeza vijana hao wanaokadiriwa kuwa zaidi ya watatu, wakamvamia na kumpiga na kitu kizito kichwani,” alisema.

 

WALIPISHANA KAULI

Baba huyo aliendelea kuzungumza kuwa mkewe huyo ambaye ndiye mama aliyemlea Amber Rutty baada ya mke wake wa awali kufariki dunia mwaka 1993, siku ya tukio alikuwa amepisha naye kauli, hivyo mkewe huyo aliondoka na mjukuu wake aitwaye Mwanaidi Ramadhani kwenda kwenye nyumba yao nyingine iliyopo jirani na eneo wanaloishi na ndipo alipovamiwa na kuuawa.

Image result for AMBER RUTTY

SABABU YA MAUAJI NI NINI?

Akizungumzia sababu za mauaji hayo, baba Amber Rutty alisema hata yeye yamemshangaza maana mke wake huyo mwenye umri wa miaka 68, hajawahi kuwa na ugomvi na mtu yeyote.

“Yaani mimi mpaka sasa sielewi kabisa kwa nini wamemfanyia unyama huo mke wangu kwa sababu ni mtu mzima sasa ana umri wa miaka 68, hakuwa na ugomvi na mtu, lakini cha kushangaza walivyompiga walichukua shilingi 8000 na simu yake ya mkononi aliyokuwa nayo,” alisema baba huyo.

 

MJUKUU ALISHUHUDIA

Akiendelea kuzungumza na Risasi Jumamosi, baba huyo alisema kuwa, wakati mkewe huyo anafanyiwa kitendo hicho cha uuaji mjukuu wake huyo mwenye umri wa miaka 12 alikuwa akishuhudia kila kitu, lakini alishindwa kupiga kelele kwa sababu walikuwa wanamtishia mapanga.

“Mke wangu ameuawa mbele ya mjukuu wake na siku hiyo hakukuwa na mtu mwingine yeyote katika nyumba hiyo zaidi ya mke wangu na huyo mjukuu.

 

“Walichofanya baada ya kumuua walimvua juba lake alilokuwa akiswalia pamoja na simu na fedha zake hizo wakaondoka na baada ya kufika mbali ndiyo mjukuu wangu huyo alianza kupiga kelele na watu wakaja na kumkuta mke wangu ameshafariki dunia ndipo walipokuja Polisi na kuuchukua huo mwili na mpaka sasa tuna majonzi sana,” alisema baba wa msanii huyo kwa uchungu.

 

KAMANDA ATHIBITISHA

Risasi Jumamosi lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Gimmin Mushi ambapo alipopatikana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea ili kuweza kuwabaini wahusika.

TUJIKUMBUSHE

Oktoba 26, mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alimtaka Amber Rutty kujisalimisha katika kituo chochote cha Polisi ikiwa ni baada ya vipande vya video zake akiingiliwa kinyume na maumbile na mpenzi wake, Said Mtopari kusambaa mitandaoni.

Baada ya kusikia tamko hilo la Makonda, Amber Rutty na mpenzi wake huyo walijisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Maturubai, Mbagala jijini Dar kabla ya kufikishwa Makahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, Novemba 2, mwaka huu kujibu mashtaka ya kufanya tendo hilo la kinyume na maumbile na kusambaza video hiyo ya ngono.

 

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Katuga amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika wanasubiri taarifa za kitaalam kuhusu picha hizo za ngono za minato. Washtakiwa hao walipatiwa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili kila mtu na kusaini bondi ya shilingi milioni 15, lakini walishindwa kuyatimiza, wakapelekwa mahabusu Segerea.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 12, mwaka huu. Wakati Amber Rutty akikutwa na msala huo na kujisalimisha Polisi Oktoba 26, mwaka huu, mama yake huyo alifariki dunia Oktoba 28 hivyo msanii huyo hakuweza kushiriki msiba huo kwa kuwa yupo korokoroni.

STORI: Imelda Mtema, Risasi Jumamosi

Comments are closed.