The House of Favourite Newspapers

Mama Wa Beki Yanga Kuzikwa Leo Mtwara

Beki wa Yanga, Juma Abdul

MAZISHI ya mama mzazi wa beki wa Yanga, Juma Abdul yanatarajiwa kufanyika leo Ijumaa mkoani Mtwara ambapo beki huyo tayari aliondoka jana kutoka jijini Mwanza kwenda mkoani huko kwa ajili ya mazishi.

 

Mama wa beki huyo aliyefahamika kwa jina la Rehema Abdul, alifariki jana Alhamisi mkoani Mtwara, huku haikuwekwa wazi alikuwa anasumbuliwa na kitu gani wakati mtoto wake akiwa jijini Mwanza ambako Yanga imeweka kambi kwa muda.

 

Uongozi wa Yanga umetoa pole kwa mchezaji huyo ambaye kwa sasa yuko kwenye kipindi kigumu baada ya kufiwa na mama yake.

YANGA SC

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mratibu wa Yanga, Saleh Hafidhi, alisema kuwa wao kama uongozi wanatoa pole kwa mchezaji huyo.

 

“Tunatarajia kuwa leo (jana) jioni ndiyo ataondoka na ndege ya jioni hapa Mwanza kwenda Mtwara kwa ajili ya mazishi ambayo yanafanyika kesho (leo) Ijumaa,” alisema Hafidhi.

 

Akizungumzia msiba huo, Abdul mwenyewe alisema: “Nilipata taarifa nikiwa Mwanza, hivyo imenilazimu kurejea Dar, ni pigo ila tunapaswa kushukuru, kuhusu utaratibu mzima jinsi itakavyokuwa, ninaamini kesho (leo) kila kitu kitakuwa wazi.”

TIMU YA HAMASA TAIFA STARS INAZUNGUMZA MUDA HUU

Comments are closed.