mama wa beyonce amkingia kifua mwanaye sakata la pesa za kampeni
Tina Knowles(70), mama mzazi wa Msanii Beyonce Knowles ameibuka na kumkingia kifua mwanaye, baada ya tuhuma za kuwa msanii huyo alilipwa pesa ili kumuunga mkono Makamu wa Rais wa Taifa hilo Kamala Harris katika kampeni za uchaguzi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tina Knowles alituma chapisho akisema “Hii imewekwa alama kwenye Instagram kama habari za uongo na kuondolewa, Inaitwa Taarifa za Uongo” na kuyakosoa majukwaa akisema “ukosefu wa uadilifu”, na kwamba ni uongo msanii huyo hakulipwa dola milioni 10 kuhudhuria kampeni hizo.
Tina alieleza kuwa “Kwa kweli Beyonce hakupokea hata senti moja kwa kuhudhuria mkutano wa mgombea urais, Makamu wa Rais Kamala Harris, huko Houston. Kwa kweli, alilipa gharama za safari yake na timu yake mwenyewe, pamoja na gharama za maandalizi yote.”
Wahanga wengine wa tuhuma hizo ni pamoja na Msanii John Legend pamoja na Oprah Winfrey, ambapo kwa upande wake John Legend alimpongeza Tina kwa kauli yake na kuthibitisha kwamba “wasanii wote walitumbuiza na kushiriki bure kwa sababu tunajali mustakabali wa taifa letu.”
Ripoti ya TMZ ilieleza kuwa Oprah Winfrey kwa upande wake yeye alisema kwamba “hakulipwa chochote” kwa kuandaa mkutano wa Harris wa “United for America” baada ya kudaiwa kuwa kampuni yake ilipokea dola milioni 1 kwa ajili ya kazi hiyo.