Mama wa Sanchi Wala Hamaindi

WAKATI mwanaye akizua mjadala kama wote mtandaoni kuwa anakaa nusu utupu kutokana na vivazi vyake, mama mzazi wa modo mwenye shepu yake Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ wala hamaindi kama kuna tatizo kwa mwanaye.

 

Sanchi ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, watu wengi wanamsema kutokana na mavazi yake, lakini kwa upande wa mama yake na watu wake wa karibu hawaoni shida yoyote.

“Mama yangu ananielewa vizuri na wala haniletei noma yoyote hivyo naona haina shida kabisa,” amesema Sanchi anayesifika kwa kutupia video na picha za nusu utupu kwenye mitandao ya kijamii.

STORI: IMELDA MTEMA,DAR


Loading...

Toa comment