Mambo 10 Usiyoyajua Kuhusu Wanawake

 

WENGI wetu kila kukicha tunajitahidi kutafuta mbinu na njia za kuwatambua wenzi watu hasa kwenye upande wa tabia na kufanya chaguo lililo sahihi.

 

Jambo la msingi ni kutambua mambo muhimu usiyoyajua kuhusu wanawake ambapo itakusaidia pia kufanya chaguo sahihi kwenye maisha ya ndoa au kwenye safari ya kutengeneza familia.

 

Mambo 10  muhimu ambayo unatakiwa kuyajua kuhusiana na wanawake na ukiyazingatia na kuyaweka akilini lazima utaona mafanikio yake siku moja ni yafuatayo:

 

1 .TAMAA ZAO

-Mwanamke yeyote anaweza kukutamani kimapenzi isipokuwa mama yako.

 

2. HULKA ZAO


-Wanawake wote huonyesha upendo wao waziwazi isipokuwa wale waliotendwa kabla.

 

3. KUACHANA


-Mwanaume kumuacha mwanamke anayempenda ni kama simba kuacha kula swala, mwanamke kumuacha mwanamme ni rahisi kama swala kumkimbia simba mzee.

 

4.  TABIA


-Jihadhari na maneno ya saluni na majirani kwamba wanaume wote wako sawa kitabia. La, lakini kumbuka hakuna mwanamme asie mwanamme.

 

5.  MPENZI WA ZAMANI


-Kujaribu kumsahau mwanamme uliyewahi kumpenda ni kama kumkumbuka mtu usiyemjua. Ni ngumu.

 

6. KUOLEWA


-Muhimu kuolewa/kuoa, na ni ngumu sana kumjua mwanamme mwema kabla ya kuoa, ni waigizaji wazuri sana. Kumbuka maneno haya,  “Muhimu kuoa/kuolewa, ukipata mke/mme mwema utakuwa na furaha, ukipata mke/mme mwovu utakuwa mwanafalsafa”.

 

7. USALITI


-Vizuri kujiandaa kisaikolojia kusalitiwa, la usipojiandaa ama unaweza kuua mtu au hata kujiua. ukiua mtu maisha yako yatakosa furaha siku zote, ukijiua mwenyewe, hao waliokusaliti wanaweza kuishi kwa furaha zaidi ya ulivyokuwa hai.

 

8.  PESA NA MAPENZI

-Mapenzi bila pesa yanapatikana kwa wingi  huko mbinguni, hapa duniani ni ngumu mno, lakini usihofu sana, kuna makubaliano bila pesa. Omba Mungu.

 

9. UONGO


-Wahenga walisema ukweli unauma, Na mimi nakuambia, “Uongo unaua”

 

10. KUWAJUA WANAWAKE


– Kutaka kumjua mwanamke kunahitaji miaka mingi ya kuishi kuliko idadi ya nywele zao. Usihangaike na vitabu, makala, majarida, filamu, nyimbo na hotuba za wanaofundisha mandhari za wanawake. Kuna kanuni moja tu ya kupenda, ” Ili ubaki salama katika kupenda sharti ujipende kwanza”.

Loading...

Toa comment