The House of Favourite Newspapers

Mambo 10 Yanayoweza Kusababisha WhatsApp Yako Kufutwa

 

MTANDAO wa kijamii, WhatsApp,  ni mmoja kati ya mitandao bora na mikubwa duniani ambayo inatumiwa kwa wingi na imeweza kuunganisha dunia kuwa kama kijiji kutokana na huduma bora walizonazo.

 

Mtandao wa Whatsapp unazo sheria zake ambazo mtumiaji hukubaliana nazo pindi anapoanza kujiunga nao kwa mara ya kwanza.

 

Yafuatayo ni mambo 10 ambayo yanaweza kusababisha akaunti yako kusimamishwa au kufutwa kabisa na wamiliki wa mtandao huo kutokana na kukiuka masharti na sheria zao.

 

10. Kutuma ujumbe wa matusi, kumchafua mtu na jumbe ambazo ni kinyume cha sheria.

Kwenye masharti yanayotolewa na mtandao huo ni pamoja na endapo utamtumia mtu jumbe wa matusi, kumchafua, kinyume cha sheria na ukaripotiwa, suala hilo linaweza likapelekea akaunti yako kuwa matatani.

 

9. Jumbe zinazochochea hatari na uhalifu.

 

8. Kufungua akaunti feki ya mtu fulani.

Endapo utafungua akaunti ya Whatsapp kwa jina la mtu fulani ambalo si lako ili kujiingizia maslahi na ikaripotiwa, basi kuna uwezekano akaunti yako ikawa kwenye matatizo ya kusimamiishwa au kufungiwa kabisa

 

7. Kutuma ujumbe mwingi kwa watu ambao haujawasajili.

Epuka kutuma ujumbe mwingi kwa watu ambao hawapo kwenye orodha ya majina yako ya simu, endapo watagundua hilo akaunti yako itakuwa kwenye matatizo.

 

6. Kujaribu kubadilisha au kuboresha code namba za Whatsapp.

 

5.  Kutuma virusi kwa watumiaji wengine.

Whatsapp pia imepiga marufuku suala la kutuma virusi kwa kutumia mtandao wake.

 

4. Kujaribu kudukua (hack) akaunti ya mtu mwingine au ya mtandao.

Endapo utagunduliwa unafanya jambo hili basi moja kwa moja akaunti yako itaondolewa na si kusimamishwa kama kwa baadhi ya makosa mengine

 

3. Kutumia Whatsapp Plus.

Endapo utakuwa unatumia Whatsapp Plus kwa taarifa ambazo unatumia kwenye Whatsapp ya kawaida basi utaondolewa kwenye mtandao huo bila kusimamishwa. Mtandao huo ulikwishatangaza kwamba hawana mahusiano yoyote na Whatsapp Plus.

 

2. Kufungiwa (block) na watumiaji wenzako.

Endapo utakuwa umefungiwa na kundi kubwa la watumiaji wenzako wa Whatsapp na mtandao huo na ukagundua hilo basi utakuwa kwenye tatizo la akaunti yako kuondolewa Whatsapp.

 

1. Malalamishi yako kuripotisha.

Endapo taarifa zako zitakuwa zimeripotiwa na watumiaji wengi, itaweza kukuletea shida kwenye akaunti yako ambayo itaweza kusimamishwa kufungiwa kabisa.

Comments are closed.