The House of Favourite Newspapers

Mambo 15 ya kukufanya uwe mama mzuri kwa mwanao!

0
Happy mother carrying her daughter at the park
1. Analofanya mwanao msapoti

Yawezekana kabisa umebaini mwanao ana ndoto za kuwa mtu f’lani katika jamii, katika mambo anayofanya kuelekea kutimiza ndoto zake mpe sapoti.
Wakati mwingine mwanao anaweza kuwaza tofauti na vile unavyowaza wewe, ikitokea hivyo kubaliana naye na wala usimbane kwa mawazo yako.

2. Mvumilie
Ukiwa mama kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kukukwaza kwa mwanao. Utakutana na changamoto nyingi lakini kwa wakati huo unatakiwa uwe mvumilivu ili uweze kumuongoza vizuri.
Kwa mfano, unaweza kubaini mwanao ameshaanza mambo ya kikubwa, yaani hasikii wala haambiwi, usiwe mkali kwake, fahamu kwamba anapitia umri f’lani unaoitwa ‘foolish age’. Kipindi hicho nenda naye taratibu.

Zungumza naye kwa upole, mueleza madhara anayoweza kupata kwa kufanya yale ambayo si wakati wake.

3. Jua anachokipenda
Mama bora ni yule ambaye anagundua haraka hobi za mwanaye. Kwa kifupi mzazi anatakiwa kujua nini mwanaye anapenda na nini hapendi.
Anapokuuliza maswali magumu wala usiwe mkali, mjibu kwa umakini kwani katika hayo anayoyapenda anatakiwa kuwa na ufahamu juu yake.

Mother and child writing/drawing...C1B3WA Mother and child writing/drawing4. Muwekee sheria na taratibu
Watoto mara nyingi ni watundu sana, sasa mzazi mzuri ni yule anayemuwekea mwanaye sheria ambazo anatakiwa kuzifuata. Kwa mfano muda wa kuamka, kazi anazotakiwa kuzifanya kwa siku na mambo mengine kama hayo.

Ukimuacha mwanao aishi ilimradi siku zinakwenda bila kumuwekea taratibu, utakuwa unakosea na huwezi kuwa katika orodha ya wazazi bora.

5. Wakati mwingine fanana naye
Ili kumuweka karibu mwanao na kumfanya asikufiche kitu, jaribu kufanana naye.
Wakati mwingine cheza naye hata michezo yake anayopenda kucheza, watoto wanafurahi sana wakipata nafasi ya kucheza na mama zao.

Mtoto akikukosea kaa naye chini na umuoneshe jinsi ulivyoumia.
Mfano jifanye unalia ili ahisi maumivu yako na kwa kufanya hivyo hawezi kurudia tena kosa lake.

6. Mheshimu mtoto wako
Njia nzuri ya kupata heshima kwa mwanao ni kumpa heshima sawa na watu wengine.
Usijaribu kumdharau kwa sababu ni mtoto, zungumza naye kwa upole na mpe heshima kama mtoto. Anapozungumza na wewe mpe nafasi ya kumsikiliza.

Itaendelea wiki ijayo .

Leave A Reply