Mambo 7 Mwanaume Hapaswi Kumfanyia Mchumba/Mke Wake.

 

Ili kuishi maisha ya amani na furaha wewe pamoja na mwenzi wako, ni muhimu kupata elimu ya jinsia na kufwata mambo ambayo ni muhimu kwenye kudumisha mahusiano yenu kama wapenzi.

Leo hii utajua mambo 7 muhimu ambayo kwa mwanaume hapaswi kumfanyia mchumba wake au mke wake.

 

1.Usimpige.

 

Kuna njia nyingi sana za kumuelekeza mtu bila kumpiga, endapo mpenzi wako atakuwa amefanya kosa epuka sana swala la kumpiga kwasababu yeye sio ngoma huwa anasikia maumivu kama wewe.

Kumbuka unapompiga kwaajili ya kosa dogo na ukazoea kumfanya hivyo, basi mwisho wa siku kuna uwezekano mkubwa ukabaki bachela kwasababu kila mwanamke atakuwa akikukimbia kwa tabia yako ya upigaji.

Tafuta mbinu nyingine mbadala badala ya kuamua kuinua mkono wako au kitu chochote na kuamua kumpiga.

 

2.Usimtukane na kumshushia heshima.

 

Epuka sana jambo la kumtukana mchumba wako matusi ya nguoni na kumshushia heshima hasa mbele za watu.

 

Unapochukua jukumu la kumtukana na kumshushia heshima mbele za watu, basi pale unamjengea swala kubwa sana kwenye akili yake ambapo moja kwa moja atakutoa katika moyo wake na atahisi kuwa hauna upendo wa kweli kwake hata kama awali alidhihirisha hilo

 

3.Usimfanye ajihisi hapendwi na anamkosi.

 

Unapofanya hatua mbili za juu, ndipo jambo la tatu humjia katika kichwa chake ‘kujihisi hapendwi na anao mkosi kukutana na wewe’

 

Epuka sana njia hizo kwasababu kichwa kikishamaliza maamuzi kinapelekea moyo na moyo ndio una maamuzi ya mwisho ambayo yanaweza yakakuharibia amani ya mahusiano yako.

 

4.Usimbake.

Baadhi ya wanaume wengi wanafikiri akiwa na mwanamke chumbani ni lazima wafanye mapenzi.Hapana.

 

Unatakiwa utumia njia mbadala ambazo zitaweza kumweka mwanamke katika vishawishi vya kutamani tendo la ndoa na sio kulazimisha kwasababu hatofurahia hali ile.

 

Kwa upande wa wenzetu wa kike wameumbwa kwa namna ya tofauti hasa linapokuja kwenye swala la mapenzi ambapo wanahitaji maandalizi makubwa nay a kutosha, endapo utafanya hivyo basi utakuwa mtu wa kupendwa na mwanamke wako hatoacha kutangaza sifa zako ambazo zitakuletea faida ya kukuongezea warembo kila kukicha

 

5.Usimsaliti na kujionyesha kabisa kwamba una saliti.

 

Baadhi ya wanaume wengine wana akili ndogo katika dunia hii kwasababu wanawaza sehemu wanapokanyaga bila kugundua kuwa wanatakiwa kusogea hatua nyingine mbele.

 

Usitumia njia ya kumvunja moyo mwanamke kwa kumsaliti huku akijua kuwa unafanya hivyo.Hakikisha pia unajua kwamba maisha ni leo na kesho, unapomtendea mtu kitu Fulani tambua kuwa na wewe ipo siku utaonja maumivu aliyosikia mwenzako.

 

6.Msikilize pale anapokua na stress, mpe muda wako, mkumbatie na mpe maneno ya faraja.

 

Kuwa mwanaume wa ukweli kwa kumpa maneno mazuri mpenzi wako, tafuta muda muulize maswali ambayo yanahitaji yeye kujieleza, jitahidi kuwa kila unapokutana naye unamwonyesha tabasamu na kumkumbatia  huku ukimpa maneno kama, ‘nimefurahi sana kukuona, nilikuwa nawaza toka jana kukutana na wewe, nakuwa na  amani ya moyoni kila nikikuona, furaha yangu huletwa na wewe, sikukosea kukupata wewe, sijui kama ntaweza kukusahau katika maisha yangu, sijui kama kuna siku ntakuwa mbali na wewe’na maneno mengine.

 

7.Mpe zawadi, hata kama ni ndogo kiasi gani kwake ni alama tosha.

 

Kuna usemi wa kizungu unasema, ‘Less Price, More Valuable’(Bei ndogo Thamani kubwa)

 

Wanaume wengi sana wamekuwa wakiwaza kuwa zawadi kwa mwanamke ni mpaka uwe na pesa nyingi ambazo unaweza kumnunulia simu, gari, laptop na vinginevyo vyenye thamani lakini sio hivyo.

 

Mwanamke anapenda zawadi inayowasilishwa kwa upendo hata kama ina thamani ndogo.

Kwa mfano; Mwanaume anaweza akampa mchumba wake gari lakini akatokea kijana mwenye upendo wa kweli anayetambua thamani ya mapenzi na akampelekea mwanamke Yule chocolate ya sh 1000 huku akisindikiza na maneno mazuri na Yule mwanamke akampenda kijana Yule zaidi ya mwanaume aliyemnunulia gari bila kumpa hata maneno mazuri.

 

Kwasababu mwanamke anaangalia yupi kati ya Yule anatambua thamani ya utu wake kwake kwahyo usifikiri pesa inaweza ikakufanya uwe juu ya mapenzi, kama ni ndio labda kwa Malaya wa muda mfupi.

 

Loading...

Toa comment