The House of Favourite Newspapers

Mambo 7 ya Kufanya Mpenzi Wako Asikuache

KILA binadamu anao udhaifu wake hasa pale anapogundua sehemu na mahali gani muhimu penye upungufu kwake na akataka kuziba pungufu lile.

Katika mapenzi endapo mwanamme atamtambua  alichokikosa mwanamke huko alipotoka na yeye akaweza kukifanya basi kutamweka mahali pazuri pa kupata penzi na upendo wa kudumu.

Kwa wanaume  wengi wamekuwa wakiachwa bila kujua shida ni nini au msichana wake kumnunia kila kukicha bila yeye kujua tatizo.  Lakini si hilo tu, pia wakati mwingine kunyimwa hata haki  ya mapenzi kwa ajili ya jambo tunaloweza kuliita ni uzembe wa mwanamme kwa ajili ya kutokutambua mpenzi wake anahitaji kitu gani.

Wanawake wote ni haki ya wanaume na kila mwanamme anaweza kutembea na mwanamke yeyote duniani isipokuwa mzazi wako na ndugu yako lakini kwa wengine wote, mwanamme anao uwezo wa kutembea nao kwa sababu tuliyoumbiwa.

Usikubali kushindwa na akili ya mwanamke kwamba huwezi kumpata, tambua kwamba wewe ni mwanamme na una uwezo mkubwa kumzidi yeye, unaweza kummiliki hata kama amekuzidi umri mpaka akawa anakuheshimu ikafikia hatua usiamini kama mambo yapo hivyo duniani.

Hayo ya juu nilikuwa tu nakukumbusha tu kwamba wewe ni mwanamme, umeumbwa kushinda na si kushindwa, mwanamke ni sehemu ya mwili wako, kwa hiyo usikubali kunyong’onyeshwa kwenye mapenzi na mwanamke.  Tumia uanaume wako, mbinu na akili yako  na si nguvu.

La msingi na la kufanya ni kujua mambo saba kwako wewe mwanaume ya kufanya ili mpenzi wako asikuache.  Hakikisha unayazingatia.

1 Hakikisha unakuwa msafi kwa kila kitu hasa unapokuwa naye.

2. Hakikisha unampa uhuru wa kutosha mnapokuwa mnafanya mapenzi, namaanisha awe na maamzi juu ya mwili wake usimlazimishe kama hayuko tayari, umuandae kabla ya kuanza kumtomasa.  La muhimu sana uhakikishe anafika kileleni kila unapofanya naye mapenzi kwa sababu hii ndiyo hatua ya mwanamke kutambua uanaume wako.

3. Umjengee mazingira ya kukuomba kufanya mapenzi anapojisikia si kufuata ratiba zako tu.

4.Usimfanye akasirike anapokuwa na wewe hata kama kakosea mweleze kwa busara na ikiwezekana uwe unahakikisha anafurahia kila jambo lako; namaanisha fanya mambo anayoyafurahia mara nyingi.

5. Kuwa mbunifu wa mapenzi kwa kumbadilishia staili mpya na ikiwezekana tumia ufundi wa ulimi ulionao kumfanya achanganyikiwe na wewe kabisa na mfurahishe kwa zawadi ndogondogo,  si lazima ziwe kubwa.

6.Msaidie kutatua shida zake za kila nyanja kadiri unavyoweza.

7.Kumbuka wasichana wana mambo mengi,  mfano kila mwezi wanaingia katika hedhi, hivyo anahitaji vifaa vya kujihudumia na anahitaji wewe umjali wakati huo.  Anahitaji kusuka, vipodozi, nguo hasa za ndani, n.k.   Hivyo,  jitahidi kuitumia karibu nusu ya pesa yako kwa ajili ya kumhudumia.

 

Comments are closed.