The House of Favourite Newspapers

Yajue mambo sita ya kukupa usingizi mnono

 

KULALA si suala la kuweka kichwa chako kwenye  mto tu; kunajumuisha mambo mengi. Ili uweze kupata usingizi mnono inakubidi kutambua na kufanya yafuatayo:

  1. Panga wakati wa kulala na kuamka

Kuanza kulala ni kitu rahisi, lakini, hata hivyo, hakikisha kwamba kila siku unaenda kulala na unaamka wakati mmoja. Kitu muhimu ni kuweka muda utakaoamka – hilo litakusaidia kuweka muda wa kulala, kwa kuwa mwisho wa siku utahisi usingizi bado una usingizi kichwani.

 

2. Ingia katika giza

Tunahitaji kutoa homoni muhimu inayokufanya kupata usingizi mwanana. Jaribu kuweka mazingira ambayo yatasababisha usingizi kama vile kuzima taa ndani ya nyumba saa moja kabla ya kulala.

 

Hiyo inamaanisha kwamba zima runinga ama kompyuta kwa kuwa vifaa hivyo vina mwangaza unaoweza kuzuia homoni ya kukupatia usingizi. Hivyo basi hufai kuona mwanga wa rangi ya buluu saa moja kabla ya kulala.

 

3.Tulia

Utulivu husababisha usingizi mwororo: Akili zetu na miili yetu inahitaji kupunguza kiwango chake cha joto hadi nyuzi joto moja ili mtu kuweza kupumzika na kupata usingizi. Hivyo basi kumbuka kuweka nyuzi za joto hadi 18 usiku.

 

4.Andaa kitanda chako kwa ajili ya usingizi

Badaa ya kufanya tendo la ndoa, mnalazimika kutulia na si kufanya kitu kama vile kusoma au kuendelea kuzungumza kwa mabishano.

 

Ubongo wa mwanadamu una kasi ya kufanya ushirikiano, kila mara unataka kushinikiza ujumbe. Kitanda ni cha usingizi si sehemu ya  kusumbuana kama mna matumaini ya kupata usingizi.

 

Iwapo umekuwa kitandani kwa dakika 20 na hupati usingizi, ondoka na kujishirikisha na mambo mengine kama vile matembezi ama hata kusoma katika chumba kilicho na mwanga mchache hadi unapohisi uko tayari kulala.

 

5. Epuka vinywaji vyenye kafeini

Kwa siku ya kawaida tunaweza kunywa kiwango cha juu cha vinywaji vinavyoongeza utandaji wetu mwilini. Punguza vinywaji hivyo saa 12 kabla ya kuingia kitandani.

 

Kafeini zinamiliki  maisha nusu: Ikimaanisha kwamba saa sita baada ya kunywa bado utakuwa na kafeini nyingi katika mwili wako hivyo,  unahitaji saa 12 ili kinywaji hicho kiondoke katika mfumo wako wa neva.

 

6.Usinywe pombe kabla ya kuelekea kitandani

Tofauti na dhana iliyopo, pombe haiwezi kukusaidia kulala ama kutulia na inaweza kuhitilifaina na mategemeo hayo njema.

Comments are closed.