The House of Favourite Newspapers

Mambo unayoweza kuyafanya kuboresha afya yako 2016

0

fitHERI YA MWAKA MPYA! Ni kawaida mtu kujiwekea malengo yake kila unapoanza mwaka, lakini kupitia kona hii ya masuala ya afya, napenda kushea na wewe mambo kadhaa unayoweza kuazimia na kuyafanya mwaka huu na kuboresha afya yako.

Elewa kwamba afya yako iko mikononi mwako, tabia ya maisha unayoishi ndiyo inayoamua afya yako iweje. Chakula unachokula ndicho kinachoamua mustakabali wa afya yako. Kama ulikuwa unayafanya haya, azimia kubadilika mwaka huu:

ACHA SODA
Unene wa kupita kiasi, kisukari, magonjwa ya moyo, figo, ini na matatizo ya kiafya mengine kadhaa, yana uhusiano mkubwa na unywaji mwingi na wa mara kwa mara wa soda. Ingawa kinywaji hiki ni kitamu na kinaruhusiwa kutumiwa na watu wa rika zote duniani, lakini tafiti zinaonesha kiafya ni miongoni mwa vinywaji vyenye hasara zaidi kuliko faida mwilini.

KULA MILO 2 KWA SIKU
Tafiti zinaonesha kuwa mahitaji muhimu ya chakula katika mwili, ni milo miwili kwa siku, ambayo unatakiwa kuila ndani ya muda wa kati ya masaa 6 hadi manane na vile vile kula mlo wako wa mwisho kwa siku hiyo, masaa 3 kabla ya kupanda kitandani kulala.

Tofauti na mazoea ya kula milo mitatu kwa siku, ulaji wa milo miwili kwa siku una faida nyingi kiafya, ikiwemo kupunguza uzito, kuzuia magonjwa, kutatua tatizo la Insulin na kinga dhidi ya uharibifu wa chembechembe hai za mwili.

Iwapo utazingatia ratiba ya kula milo miwili kwa siku ndani ya muda huo wa masaa sita mpaka manane, pamoja na kuzingatia suala la kuhakikisha mlo wako wa mwisho usiku unakula angalau masaa matatu kabla ya kulala, unatakiwa uchague mlo mmoja wa kuacha kula.

Kwa kawaida kuna milo mitatu kwa siku, ambayo ni kifungua kinywa cha asubuhi (breakfast), chakula cha mchana (lunch) na chakula cha usiku (dinner), hivyo iwapo utafuata utaratibu wa milo miwili kwa siku huna budi kuchagua kati ya kula mlo wa asubuhi na mchana, au kula chakula cha mchana na usiku tu na usichague mlo wa asubuhi na jioni.

Hii ina maana kwamba ulaji mzuri wa milo miwili kwa siku wenye faida kiafya ni ule wa ama kula mlo wa asubuhi na wa mchana usiku ukaacha au wa kula mchana na usiku na asubuhi ukaacha. Haishauriwi kula mlo wa asubuhi na ukaacha wa mchana hadi usiku.

naweza kuchelewesha mlo wa asubuhi ukaula pamoja na wa mchana na ukamalizia na mlo wa usiku, ndani ya muda wa masaa sita hadi manane na ni lazima chakula cha usiku ukile mapema, masaa matatu kabla ya kulala ili tumbo lipate muda wa kusaga chakula.

PATA USINGIZI SAA 8 KWA SIKU
Usingizi ni kitu muhimu katika afya ya binadamu. Mtu mzima anapaswa kupata usingizi usiopungua saa sita hadi nane kwa siku.

Ukosefu wa usingizi wa kulala saa chache kuna athari katika afya yako, kwani kunadhoofisha kinga ya mwili na kunakuweka katika hatari ya kupatwa na magonjwa mengine hatari.

Bila shaka maazimio hayo yako ndani ya uwezo wako, chukua hatua ya mabadiliko kwa ajili ya afya yako.

Leave A Reply