visa

MAMBO YAKUZINGATIA IWAPO UNATAKA KUSHIKA MIMBA

WanaWake wengi wanapenda kushika mimba lakini baadhi yao hawashiki. Sio kwa mapenzi yao, hivyo leo tutashauri nini cha kufanya ili upate mimba. Mayai ya mwanamke ni mojawapo ya viungo ambavyo vimeshatengenezwa kabla hata mwanamke hajazaliwa, yaani tangu akiwa tumboni mwa mama akiwa kiumbe kiitwacho kitaalamu fetus.

 

Haya mayai yanakuwa tayari pale msichana anapopata hedhi  yake ya kuanzia akiwa na miaka kati ya 12 mpaka 14 hadi pale atakapofikia kikomo cha kupata hedhi kitaalamu huitwa menopause menstruation. Ukomo wa hedhi ni kuanzia miaka 51 mayai yake na fertility yake hupungua anavyozidi kuzeeka. Yaani katika ujana wake, akiwa na miaka kuanzia miaka 14  ni muda ambao ni rahisi kutunga mimba.

Kuanzia miaka 30 had 51 uwezo huo unapungua kwa kiasi kikubwa mpaka unapoisha kabisa. Wakati kwa wanaume wao huanza kutoa mbegu pale anapobalehe na huwa hivyo hadi siku ya mwisho wa maisha yake. Hii inamaanisha kama mwanaume akiwa katika hali nzuri ya kiafya anaweza kumpa mimba mwanamke hata akiwa mzee wa miaka 80 au zaidi.

 

Mambo yanayosababisha mwanamke asipate mimba yapo mengi.

 

Moja, ingawa unene unaweza kumzuia mtu asishike mimba lakini kufanya mazoezi sana na kuwa na uzito mdogo sana wa chini ya kilo 40 huweza pia ushika mimba.

 

Dk. Marise anapatikana Marise Dispensary, njia panda ya Mabibo mkabala na kituo cha mafuta. Simu: 0713 252394. kumsababisha mtu asishike mimba. Mazoezi ya kupindukia huathiri homoni mwilini.

 

Pili, kuwa na msongo wa mawazo ‘stress’ huweza pia kuathiri uwezo wa mtu wa kushika mimba.

 

Tatu, kutokula vizuri na kutopenda kula kwani humkosesha mwanamke au hata mwanaume baadhi ya virutubisho muhimu vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanikisha suala la kushika mimba.

 

Nne, Sigara, dawa za kulevya kama bangi, pombe ni miongoni mwa vitu ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa kubeba mimba.

 

Mwanamke anayetaka kubeba mimba anashauriwa aache kunywa pombe na kuvuta sigara. Mwanaume pia anashauriwa kuacha kuvuta sigara kwani sigara huathiri kiwango cha mbegu za kiume za mwanamme.

 

Tano, endelea tu na tendo la ndoa bila kuchoka au kukata tamaa, lakini ni bora nguvu zihifadhiwe kwa siku chache kabla ya hedhi au Ovulation na siku kadhaa baada ya hapo ili mwanaume aweze kuboreshe na kuhifadhi mbegu zake kwa ajili ya siku hizo.

 

Sita, kulala kwa dakika kadhaa baada ya tendo la ndoa huongeza uwezo wa mbegu ya kiume kuweza kuendelea kukutana na yai la kike na hivyo kuongeza uwezekano wa kubeba mimba.

Saba, jiepushe kunywa kahawa na vinywaji vyenye caffeine kwani huweza kukuongezea matatizo ya kushindwa kushika mimba.

Nane, jiepushe na kutumia dawa za aina yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinazonunulika maduka ya dawa bila ulazima wa cheti cha daktari au Over-the-counter drugs inabidi zitumiwe baada ya kushauriana na daktari.

 

Tisa, usitumie baadhi ya vitu vinavyoufanya uke uwe na hali itakayoua mbegu za kiume au kupunguza majimaji yake. Vitu hivi ni kama pafyumu mbalimbali na tampons zinazotumiwa na wanawake ili kuufanya uke uwe na harufu nzuri au mafuta ya aina mbalimbali na jeli kwa ajili ya kulainisha sehemu za siri, mafuta ya kula (vegetable oils) glycerin na mate visitumike kupaka sehemu za siri.

 

Vitu hivi kufanya Ph ya uke isiwe ya kawaida na huweza kuua mbegu ya kiume, kusababisha baadhi ya magonjwa ya wanawake au kupunguza majimaji ya ukeni ambayo yanatakiwa ili kusafirisha mbegu za kiume.

 

Kumi, hakisha mwenza wako hafanyi kazi katika mazingira yenye mada hatari ambazo hupunguza uwezo wa mbegu za kiume au kutungwa mimba. Kwa ushauri zaidi wasiliana na mtaalamu wako.
Toa comment