The House of Favourite Newspapers

Mke wa Aliyetobolewa Macho na Scorpion Atoa Ushahidi Mahakamani

scorpioni-1

scorpioni-2

Salum Njwete ‘Scorpion’ akiingia Mahakama ya Mwanzo Ilala, Dar.

scorpioni-3

Scorpioni (mbele) akitoka mahakamani chini ya ulinzi mkali wa Kikosi cha Sskari Magereza.

scorpioni-4

scorpioni-5

Mke wa Saidi Mrisho aliyetobolewa macho, Stara Sudi (katikati) akiambatana na ndugu pamoja mdogo wa mumewe,  Yahaya Kisukari ambapo wote wawili wametoa ushahidi wao mahakamani hapo..

scorpioni-6

…Akiingizwa kwenye gari kurejeshwa Gereza la Ukonga.

Na Issa Mnally

DAR ES SALAAM: Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi kwa kumtoboa macho, Saidi Mrisho inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ leo iliendelea kwenye mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini hapa ambapo mke wa aliyetobolewa macho, Stara Sudi na mdogo wa majeruhi huyo, Yahaya Kisukari walitoa ushahidi wa tukio hilo mahakamani hapo.

Wanahabari wetu wakiwa kwenye viunga vya mahakama hiyo majira ya saa mbili asubuhi Scorpion alifikishwa mahakamani na kuingizwa kwenye mahabusu ya mahakama hiyo kwa ajili ya kusubiri kesi yake kutajwa.

Ilipofika saa tatu na nusu mtuhumiwa huyo alipandishwa kizimbani mbele ya hakimu Flora Haule ambapo Wakili Mwandamizi wa Serikali aliielezea mahakama hiyo kuwa kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya mashahidi wawili wa upande wa serikali.

Baada ya kuweka wazi hayo kwa kuwa shahidi wa kwanza alikuwa ni majeruhi mwenyewe ambaye alishatoa ushahidi wake kesi iliposikilizwa mara ya mwisho hivyo leo ilikuwa ni siku ya shahidi wa pili, Stara Sudi na ambaye ni mke wa   majeruhi na shahidi wa tatu Yahaya Kisukari ambaye ni mdogo wa majeruhi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 11, 2017 itakapotajwa tena ambapo mashahidi wengine wa upande wa serikali watatoa ushahidi wao.

Comments are closed.