Mambo yanayofurahisha faragha-2

042514HealthHappyCouplesCuddleatNightKWANZA nianze kwa kuwashukuru wafuasi na wasio wafuasi wa vyama vya siasa nchini kwa kumaliza uchaguzi mkuu kwa amani.

Kwa uchaguzi huu nimejifunza kitu kuwa kumbe Watanzania tunu yetu kubwa tuliyojaliwa na Mungu ni amani, amani ndiyo imenifanya leo uweze kusoma mada hii ya mambo yanayofaa faragha

Wiki iliyopita tulizungumzia kipengele kimoja cha sauti za kubembeleza leo nitaendelea na mambo mengine mazuri mnapokuwa faragha;

Busu
Kama ulikuwa hujui busu ni zuri mnapokuwa faragha kwani linahamasisha sana kinyang’anyiro chenu, wakati mwingine ukipiga busu lililozuri linaweza kuwa ni kumbukumbu kwa mwenza wako kwa muda mrefu.

Deko
Kudeka hasa unapokuwa faragha ni poa sana kwani inaonesha ni namna gani unajisikia furaha, amani, upendo kuwa na mtu ambaye ukimdekea anakufariji na kukubembeleza, ni nzuri hii kwa uhusiano, haijalishi cheo chako, umri au uwezo ulionao.

Minong’ono
Sauti za mahaba huwa ni zile za kunong’onezana zenye kujaa matamshi ya kubembelezana, minong’ono hiyo huhamasisha sana mnapokuwa faragha hasa baada ya kumaliza ngwe ya kwanza na kuitafuta ya pili.

Pongezi
Wengi hujisahau sana kutoa pongezi kwa wapenzi wao mara baada ya kumaliza tendo husika na matokeo yake wanakuwa kama vile wana ugomvi, mkimaliza kazi mwambie mpenzi wako, baby pole kwa kazi nzito uliyofanya.

15_forgotten_habits_of_happy_couples_01Furahia
Pongezi pekee hazitoshi kama unahisi umefurahia huduma yake , mwambie kabisa ili na yeye ajue amefanya kazi nzuri aliyopaswa kufanya na hata kama hajafanya vizuri mwambie ukweli ‘ ila mai kwa leo mimi sijainjoi wangu, haikuwa kama siku ile…’’

Valishaneni
Kama mliweza kushirikiana mwanzoni mwa zoezi kwa kusaidiana kutoa sehemu ya nguo zenu, vivyo hivyo mnapaswa kushirikiana pia katika kuvalishana mara baada ya kumaliza zoezi lenu.
Kimsingi mapenzi ni uwezo binafsi lakini pia ni suala la utundu na ujanja wa mtu katika kuhakikisha anaweza kumfikisha mwenza wake mahali anapohitaji kufika kwa maana ya kufikia kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Mpenzi msomaji usikose mada nyingine tamu wiki ijayo, pia usikose kufuatilia ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook na WhatsApp kujua mengi kuhusu mapenzi.
Toa comment