Mambo yanayofurahisha faragha

Relationships-Happy-Couple (1)ASANTE Mwenyezi Mungu kwa Jumatatu hii murua. Baada ya vuta nikuvute ya uchaguzi mkuu, hatimaye jana Watanzania tumetumia haki yetu ya kimsingi na kikatiba kumchagua kiongozi tumtakaye atakayeiongoza Tanzania kwa awamu ya tano.

Tukiachana na siasa, tunakutana tena katika kilinge chetu hiki kama ilivyo ada, bado tunaendelea kujifunza namna mbalimbali ya kufanya tunapokuwa faragha na wenza wetu. Kwa kifupi mada hii ya faragha imewavutia wengi sana ambao wameomba niendelee kuifafanua zaidi.

Nianze kwa kusema kila kitu kinahitaji hamasa au hisia ili kiweze kufanyika katika hali nzuri, ndivyo hivyo hata mapenzi nayo yanahitaji hamasa ili kuweza kuamsha hisia za mwenza wako na hatimaye kukutana faragha. Mnapokuwa faragha kuna kipindi inabidi mpongezane kwa kazi nzuri mliyoifanya ya kuhakikisha kila mtu anafurahia faragha yenu.

Happy couple bedLeo nitazungumza kuhusu umuhimu wa vitu mbalimbali vinavyoweza kuifanya faragha yenu kuonekana ni nzuri na bora zaidi. Kuna vitu vingi ambavyo vinapaswa kufanyika ili kukamilisha faragha yenu kuwa yenye tija, baadhi yake ni kama ifuatavyo;

SAUTI YA KUBEMBELEZA
Ikumbukwe kwamba sauti ya mtu akiwa anazungumza wakati mihemko au mizuka haijampanda huwa ni sauti ya kawaida na inapotokea mihemko imepanda basi hubadilika, hiyo inayobadilika ndiyo ninayoizungumzia.

Kuna sauti f’lani za mahaba ambazo husikika watu wanapokuwa wamezama zaidi kwenye dimbwi zito la mahaba. Mfano; baadhi ya wanawake wamejaliwa kuwa na sauti f’lani za furaha au raha na zenye kuhamasisha wanapokuwa faragha na wenza wao, kiukweli sauti hizo zinastahili kuwepo ili kumhamasisha mwenza wako.

Sauti hizo za mahaba siyo tu kwa wanawake, hata kwa wanaume pia.
Kusikika kwa sauti hizo za mahaba hata kama mwenza wako atakuwa amechoka pindi anapozisikia au kuzifikiria sauti zile akilini mwake basi anapata nguvu mpya ya kuingia tena ulingoni.

Japokuwa kila mwanadamu ameumbwa na aina yake ya hamasa anapokuwa faragha, kwa hiyo kama hatakuwa na sauti za mahaba, basi anaweza kuwa na kitu kingine zaidi.

Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook na WhatsApp kujua mengi kuhusu mapenzi.
Mada hii itaendelea wiki ijayo.


Loading...

Toa comment