Mambo Yazidi Kunoga, Wananchi Sasa Kunufaika na Magift ya Kugift Awamu ya Pili

Dar es Salaam, 5 Desemba 2024: Kampuni ya mtandao wa simu wa YAS Tanzania imezindua kampeni ya Magift ya Kugift Awamu ya Pili kwenye kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Yas Biashara, Isack Nchunda, amesema;
“Leo, tunajivunia kuzindua awamu ya pili ya kampeni hii, tukijikita zaidi katika kuwafurahisha wateja, mawakala, na wafanyabiashara wetu.

Awamu hii inaleta msisimko mkubwa zaidi, na kilele chake ni zawadi kuu ya gari jipya aina ya Kia Sorento pamoja na shilingi milioni 50 kwa wateja wawili watakaobahatika.
Kampeni hii siyo tu kuhusu kutoa zawadi au Kugift, bali ni ishara ya shukrani zetu za dhati kwa uaminifu na mchango wenu katika safari yetu ya kuboresha maisha ya kidijitali ya Watanzania kupitia Mixx by Yas.
Aidha Nchunda amesema katika awamu ya kwanza ya kampeni hii, tumegusa maisha ya maelfu ya wateja wetu, mawakala na wafanyabiashara.
Tumewatunuku zawadi zenye thamani kubwa, ikiwa ni pamoja na shilingi milioni 84 zilizogawiwa kwa washindi mbalimbali na simu janja 126.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa Yas, Edwardina Mgendi, amesema wateja wanachohitajika tu kufanya muamala wowote kupitia Mixx by Yas au kununua kifurushi cha Yas. Kila muamala unaongeza nafasi ya kushinda zawadi hizi kubwa.
Kwa mawakala na wafanyabiashara, juhudi zenu zinatambuliwa na tunahakikisha kwamba mnapata zawadi za kila wiki kwa kufikia malengo ya miamala iliyowekwa.
Kwa miaka thelathini, tumekuwa pamoja tukijenga msingi wa huduma bora na zenye ubunifu.
Mixx by Yas haisimami tu kama huduma ya kifedha, bali pia kama mshirika wa kweli wa maisha yako ya kila siku.
Kupitia kampeni hii ya ‘Magift ya Kugift,’ tunataka kuimarisha mshikamano wetu na kushiriki furaha ya msimu huu wa kipekee.