The House of Favourite Newspapers

MAMBOSASA AFUNGUKA ASKARI ANAYEDAIWA KUMUUA AKWILINA -VIDEO

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema askari aliyefyatua risasi iliyomuua Akwelina Akwelini, bado hajatambulika kwa sababu askari walikuwa wengi wala silaha iliyotumika haijajulikana, hivyo jeshi hilo linaendelea na upelelezi.

 

Mambosasa ameyasema hayo leo Machi 30, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar.

“Ikumbukwe kuwa, askari waliyotuhumiwa kuhusu kifo cha Akwilina walivyokamatwa tulieleza bayana kwamba upelelezi unafanyika ili kujua ni nani ambaye ametenda kosa lile. Silaha moja ambayo haijajulikana ni ipi ndiyo iliyomgusa Akwilina, bado tunaendelea na upelelezi, hakuna ushahidi ni askari yupi alihusika maana walikuwa wengi,” amesema Kamanda Lazaro.

 

Comments are closed.