The House of Favourite Newspapers

Mambosasa Azungumzia Wanaodaiwa Mabaunsa wa Kuchafua Uchaguzi

 

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amefunguka kuwa amepata tetesi kuwa kuna mabaunsa wanaodaiwa wameletwa jijini Dar kwa nia ya kuvuruga uchaguzi mdogo wa ubunge wa Kinondoni utakaofanyika kesho, Feb 17, 2018.

 

Mambosasa ameyabainisha hayo leo wakati akizungumza na wanahabari huku akiwatoa hofu wananchi kuwa jeshi lake limejiandaa vizuri kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi huo na kuwaonya waliopanga kufanya vurugu kuwa watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

 

“Nimeambiwa kuna mabaunsa wameletwa kwenye uchaguzi huu, mimi sijawahi kuona baunsa anayeweza kushindana na Serikali. Aliyejiandaa kupambana na Dola namuonea huruma sana, hatabaki salama.

 

“Niwaambie tu kwamba, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limejipanga vizuri kuimarisha ulinzi na usalama. Tutahakikisha usalama unakuwepo, hakuna atakayefanya vurugu wakati wa uchaguzi,” Kamanda Mambosasa alisema.

Comments are closed.